Ilikuwaje mara ya kwanza ulipokutana na mtu mliyechati mtandaoni kwa nia ya kuwa wapenzi?

Iliwahi kunitokea mimi pia. Zamani hizo hapahapa JF niliandika nataka mtoto wa kufanya nae mambo ya kikubwa tu. No serious relation.

Dada mmoja akanisakua kwenye mawasiliano niliyoweka. Tukabadilishana phone no. Tukaanza kuchati. Nilikuwa chuo kipindi hiko. Ikatokea nae kumbe alikuwa chuo cha kati mkoa uleule niliokuwa mimi.

Tulichati visiku kadhaa kwa mahaba yote. Hatimaye siku ya siku ikampendeza mola tukutane.

Nilipanda gari hadi kwenye chuo alichokuwa anasoma. Njiani tulivokuwa tunawasiliana alionekana yupo very exited kuniona, ila nilivofika duh!.

Sawa hakunichana, ila unaona tu kabisa mtu huyu kakutana na mtu ambaye hakumtarajia. Tulipiga story mbili tatu mi mwenyewe tu nikaona huu ugeni umeenda ndivyosivyo nikaaga nikaondoka.

iLa baadae usiku nilivojaribu ku initiate contact nae ndo akanichana sasa. Kwamba hakutarajia mtu kama mimi ndiye alikuwa anamngoja. So lets end it here na tufanye kama hamna kitu kimetokea.

Kutokana na haya ma sosho media, juzijuzi nimemfuma anatangaza biashara yake Facebook. Si unajua tena wadada siku hizi na tubiashara biashara. Kaweka na namba yake Tena yupo mkoa huu huu ninaoishi. Sijapata tu muda, ila i hope ntamtimbia siku moja japo tukapige tu story.
 
Nina scenario 2 kama ifuatavyo,

Scenario 1
"Mhhh mbona katoto, ndo huyu kweli?" Alisema mwenzie aliyekuwa nae pembeni kwenye gari. Binafsi nilipoteza confidence na nikazuga tu kuwa nitawachek muda kidogo kuna assignment nafanya hiyo ni miaka fulani nikiwa napiga shule IFM, kwa kweli nilidharirika sana, uzuri tu ilikuwa usk hakuna aliyeshuhudia.

Scenario 2
Anapiga simu mdada mwenye sauti nyororo anajitambulisha kwa jina X, nampokea kwa bashasha ananiambia mm ni yule tunawasiliana sana kwenye messenger nadhani ni hotmail by then. Basi kidume bahati ilioje nikawa nipo kikazi Moro so nikamwambia namaliza session then napanda gar saa 8 kumfuata Dar, akaniambia poa tukakubaliana achukue lodge pale ubungo ili iwe rahisi mm asbh kudaka gar kurudi zangu Chugastan.

Nikaelekezwa lodge hadi room Number, chap nikafika nikagonga mlango mtu huyo...nikawa najaribu kumtazama aisee nikawa najarb kuinama nimuangalie vzr lkn kiukweli ni wale wadada wa mdomo wa sungura dah ilini-stress sana nishaingia ndani na natokaje sasa...anyway tuishie hapo.
 
Umenikumbusha nyimbo ya Rupert Holmes inaitwa Escape,(Pina Colada)

Rupert alikua kachoshwa na mke wake,akaamua atafute mwanamke MWINGINE amuoe,time hiyo hakukua na Simu Wala fb,so akanunua Gazeti kaficha utambulisho wake,akaweka tangazo kua anatafuta mwanamke,sifa asiwe smart sana awe na half brain,asiwe mlevi,hata kama anapenda yoga sio mbaya,Cha mwisho awe anapenda Pina colada (aina ya chakula)..

Akatokea mwanamke ambae ana sifa kama zile,nae kachoshwa na gume gume lake,wakapanga date kukutana,siku ya kukutana kaenda kukutana na mke wake.. wakachukuana wakarudi home..
 
demu anayekaa Masaki ni mrembo kulingana na nguo na vipodozi anavyotumia.

demu anayekaa Chalinze ndani ndani ni Mzuri wa asili.

kwani huyo demu anayekaa Masaki anazaliwa na Malaika au Eliens?
Ndugu Kitombise urembo huanza kwanza na lishe bora. Watoto wa Masaki na Oysterbay ni wazuri kuliko wa uswazi kwa sababu ya lishe. Virutubisho ni muhimu sana. Njaa ni kitu kibaya sana. Inaharibu hata sura za watu. Mtu mwenye njaa ana sura mbaya ambayo pia huchangia kuwa na roho mbaya.
 
Ulikuwa una sura mbaya?
 
sawa sawa
 
Mimi scenario yangu ilikuwa tofauti kidogo maana niliiba number ya demu Kwenye simu ya rafiki yangu mmoja.

Ipo hivi, siku Moja tulikuwa kijiweni tunacheza draft then rafiki yangu mmoja akanipa simu yake nimfanyie settings ilikuwa inamzingua.Simu yenyewe ilikuwa ya buttons ya Itel,Sasa baada ya kufanya settings chap nikakimbia Kwenye inbox ya jamaa nikaanza kusoma messagesπŸ˜‚

Kwenye charts nikaona jina la mtoto mmoja anaitwa Sharon.
Nikaiba number yake nikaisave Kwenye simu yangu nikasema ngoja nimjaribu huyu.
Nilipofika nyumbani nikaa nyuma ya keyboards za simu yangu nikaanza kuchart na mtoto Sharon.
Nilitongoza mtoto akajaa mazima ikabaki ishu ya kukutana tu.Kumbe mtoto kwao na kwetu sio mbali kihivyo.

FAST FORWARDING: Mtoto alinipa location nikaenda nikakutana naye nikakuta Ni mtoto mzuri balaa.Sura nzuri na nyuma kajazia vizuri.

Picha linaisha nilikula Sana yule mtoto ila rafiki yangu hakuwahi kustukia mchezo wetu.
Tulidate almost for 1 year then tukaachana jumla kila mtu akashika njia yakeπŸ˜‚

I hereby rest my case.
 
πŸ˜…πŸ˜…Nilikuwa nimechokachoka tu, hata dress code yangu mi mwenyewe ilinisaliti baada ya kukutana nae. Nilikuwa mwanafunzi obviously sikuwa na hela.
Kupigika kifedha = kuwa na sura mbaya. Demu akishaona umechoka anakuona kama sokwe mbele yake. Hata mimi siku nakutana na huyo manzi nilikuwa nimevaa suruali ya kitambaa na shati kama la mwanakwaya wa kijijini kwa kina Lucas Mwashambwa. Hata kukutania pale Njiro Complex ilikuwa ni kufosi mambo.
 
Moja ya vitu sipendi basi ni kukonda aisee.
Ukikonda kwa njaa unaonekana tu.

Nimeishi Mbeya, Iringa, Shinyanga, Tanga na Dsm. Kati ya mikoa yote hiyo Dsm ndo inaongoza kwa vijana kukonda kwa lishe duni.
Unamkuta mwanachuo kapendeza ila sura haina nuru, mwili umekongoroka mno, tumbo limeingia ndani mpaka imekua kama ana kibiyongo.

Mavazi ni muhimu ila wanachuo mzingatie chakula sio kuwaza mavazi tu.
 
Hebu tuache kidogo basi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Na
Na mkaachana?
 
Hujakoma tu au bado unaendelea kukutana nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…