Imagine kijana wa miaka 23 anakimbizana club wakati Hana kazi ya maana

Duuh mbona Hatari!
 
Inawezekana uko sahihi ila sababu zako ulizotumia kujenga hoja yako ya kwamba vijana wa miaka hiyo hamnazo ni za kawaida sana.

Hasa hiyo hoja ya kwenda club ilihali huna kitu, hata sisi vikongwe tumefanya hiyo (ni kawaida ya maisha ya ujana hasa ukiingia chuo pale ile mindset ya Bata ulilokua unaambiwa utalikuta chuo inajaa kichwani)

Kuamini maisha simple ni kawaida kwa Kila kijana ambae bado haujaingia field kwa miguu yote, so anahisi muda wowote anaweza kutoboa.

Kuishi nyumbani, kwa umri wao ni sawa kwasababu umri huo wengi wao bado wako mavyuoni huko.

Kutokufuatilia mambo ya siasa, ni lifestyle kwa maana Kila mtu anachokitu kinachomlia muda wake kukifuatilia, kuna wazee wengi sana ambao hawajui chochote kuhusu hayo mambo so si jambo linaloweza kupima akili ya mtu.

So, kama hizi ndio sababu zilizokufanya uamini hivyo kwangu Mimi naona kama hazina nguvu sana, ila kama zipo nyingine lete maneno mkuu.
 
Hao vijana walijizaa wenyewe? Ukiona kijana mbumbumbu ujue wazazi pia mbumbumbu.
 
Hii ni hatari na nusu.
 
Jibu la Swali lako lipo katika Makala hii, nilishapita hatua ya kujiuliza hilo swali nikaenda kwenye majawabu

 
Hayo ni matokeo ya malezi mabovu kwa mtoto
 
Hamna Mkuu.
Kilichopo sasa hivi kilikuwepo tangu siku ya Kwanza binadamu anaumbwa.

Binadamu ni yuleyule.
Ukisikia mtu anakuambia binadamu wa zamani na sasa ni tofauti ujue anakudanganya
Mkuu linganisha walimu wa miaka ya nyuma walivyokuwa wakiheshimika, na walivyokuwa wakipenda kazi yao.

Pili wanafunzi walikuwa hawazidi 45 Kwa darasa.

Linganisha na aina ya walimu tulio nao sasa, na mlundikano wa wanafunzi kwenye madarasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…