Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Wadau hamjamboni nyote?
Taarifa hapo chini:
Mtoa hotuba wa Ijumaa ya leo msikiti Sunni Dodoma (Nunge) Imamu sheikh Mbwana Haji amesema muislamu anapaswa kujipamba na tabia njema wakati wote na kamwe hatakiwi kufanya ubaya ikiwa watu wengine wanafanya ubaya kwake au kutoa kauli mbaya mbele yake.
Akiongea kwenye hotuba ya leo amesema muislamu anatakiwa aigwe na wemgine na yeye asifuate mkumbo wa watu wasio na maadili mema.
"Watu wema hawatukani watu wanaowatukana wao. hawarudishi kauli mbaya kwa kauli au matamko mabaya. Bali wao hukaa kimya na kutoa nasaha. Vinginevyo ukikabili kila ubaya kwa ubaya maisha yatakuwa fujo tu kwa sababu ubaya upo kila mahala. Mambo mengine yaache yapite na lazima waislamu kazi yao iwe kuzima ubaya" Amesema.
Nkussa Online