Imamu sheikh Mbwana Haji - muislamu anapaswa kujipamba na tabia njema wakati wote na kamwe hatakiwi kufanya ubaya ikiwa wengine wanafanya ubaya kwake

Imamu sheikh Mbwana Haji - muislamu anapaswa kujipamba na tabia njema wakati wote na kamwe hatakiwi kufanya ubaya ikiwa wengine wanafanya ubaya kwake

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa hapo chini:

Mtoa hotuba wa Ijumaa ya leo msikiti Sunni Dodoma (Nunge) Imamu sheikh Mbwana Haji amesema muislamu anapaswa kujipamba na tabia njema wakati wote na kamwe hatakiwi kufanya ubaya ikiwa watu wengine wanafanya ubaya kwake au kutoa kauli mbaya mbele yake.

Akiongea kwenye hotuba ya leo amesema muislamu anatakiwa aigwe na wemgine na yeye asifuate mkumbo wa watu wasio na maadili mema.

"Watu wema hawatukani watu wanaowatukana wao. hawarudishi kauli mbaya kwa kauli au matamko mabaya. Bali wao hukaa kimya na kutoa nasaha. Vinginevyo ukikabili kila ubaya kwa ubaya maisha yatakuwa fujo tu kwa sababu ubaya upo kila mahala. Mambo mengine yaache yapite na lazima waislamu kazi yao iwe kuzima ubaya" Amesema.

Nkussa Online

1724707069260.jpg
 
Mimi sio Muisilamu, na kwa mafundisho hayo, kama waislame wote wangekua hivyo, watu wengi wangeuona uhisilam ni mzuri lakini mambo ni tofaui ktk Jamii.
nawatakia watu wote kumjua Mungu na kua lugha njema na upendo kwa wote.
 
Kuna Waislamu wanaishi hivi kama anavyohubiri Sheikh. Tunaishi nao, tunakula nao, matatizo yao ni yetu ni yao na yao ni yetu. Miaka inaenda tumekuwa wakubwa sasa na hakuna kilichobadilika.

CHUKI NI KWA AJILI YA WATU DHAIFU, WATU IMARA HUCHAGUA UPENDO.
 
Back
Top Bottom