Imekuwaje mpaka PSG ameruhusiwa kutengeneza timu iliyokamilika namna hii?

Imekuwaje mpaka PSG ameruhusiwa kutengeneza timu iliyokamilika namna hii?

Barcelona ya sasa hawategemei kupossess tu kama umeangalia games zao chini ya Flicks utagundua kuwa wana mpira wa kasi pia kwenda goli la mpinzani​
Ni kweli but maana yangu ilikuwa ukiwapokonya kupossess ni rahisi sana kuwafunga maana kujilinda hawako vizuri sana kama PSG so siraha yao hasa ni kumiliki mpira.
PSG hata ukiwapokonya possession huoni unawafungia wapi at the same time full backs zao zote mara nyingi ndo zinazopeleka mashambulizi yakushtukiza mbele rejea game na Bayen munich, Bayen walikuwa wanamiliki sana mpira ila hatari chache sana wakati wao mipira miwili au mitatu ya hatari wanakuadhibu na mara nyingi wanakufunga goli za mapema kukivuruga.
Luis kaitengeneza ile timu kimbinu zaidi inatakiwa kuwe na kocha wakutegua hizi mbinu na si kutegemea maamuzi ya mchezaji mmoja mmoja kama wanavyofanya Madrid.
 
Ni mwembamba kwa Sababu hakuna timu pale ni jina tu limebaki
Ndicho kitu ambacho Mashabiki maandazi huwa hawataki kusikia kabisa, wanadhani ukubwa wa jina na mafanikio ya Real Madrid ni kila mwaka, kumbe kuna zama ambazo Wachezaji hushuka viwango ilihali timu zingine huwa vizuri kiusajili na makocha bora kutoa upinzani kama kilichomkuta leo dhidi ya PSG.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Hukuangalia mpira, mi mwenyewe nilikuwa upande wa PSG ila niliteseka sana.
Unavyopumbazwa navyo hapo ni ball possession, total passes na pass accuracy, nakati hata back passes huwa zinajumuishwa ktk ball possession, acha ubishi wa Waha au Wapemba ili upate maarifa zaidi Mkuu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Sawa!
PSG dhidi ya Aston Villa iliteseka sana na ilipaki basi.

Tayari mkongwe, nimeacha ubishi.
 
😂😂😂
Utasema hatuna macho, huyo mtoto wa kidachi anapoteza mali hatari.

Kama kiungo chao kilishindwa kuwaka kwenye game zote mbili za Inter kitawezaje kuwaka dhidi ya PSG!?

Chief hii backline ya PSG imeshakutana na Arsenal, imeshakutana na Liverpool, imeshakutana na Bayern, imeshakutana na Inter, imeshakutana na Real Madrid leo.
Sidhani kama tunaidai.

Bila kusahau, huyo Lamine Yamal juzi tu hapa ametoka kupigwa kufuri na Nunes (Portugal vs Spain).
Timu zote za ligi 4 bora kazipopoa. SPAIN,ITALY,ENGLAND na FRANCE kwenyewe ndo hawataki kuisikia, wamebeba makombe yote.Tukubali jamaa wako form mwaka huu.
Chelease mwenyewe anatakiwa kupambana ili achukue hilo kombe..akienda kichwakichwa atapgwa.
 
Namlaumu sana Alison Becker, kuna kitu ametunyima kwenye kuizungumzia PSG!
Sijui alitumia mzizi gani yule mbwa kwenye ile game!?
 
Ni kweli but maana yangu ilikuwa ukiwapokonya kupossess ni rahisi sana kuwafunga maana kujilinda hawako vizuri sana kama PSG so siraha yao hasa ni kumiliki mpira.
PSG hata ukiwapokonya possession huoni unawafungia wapi at the same time full backs zao zote mara nyingi ndo zinazopeleka mashambulizi yakushtukiza mbele rejea game na Bayen munich, Bayen walikuwa wanamiliki sana mpira ila hatari chache sana wakati wao mipira miwili au mitatu ya hatari wanakuadhibu na mara nyingi wanakufunga goli za mapema kukivuruga.
Luis kaitengeneza ile timu kimbinu zaidi inatakiwa kuwe na kocha wakutegua hizi mbinu na si kutegemea maamuzi ya mchezaji mmoja mmoja kama wanavyofanya Madrid. Nashindwa kuelewa Liverpool alitowaje kwa penalt na hawa kenge.
 
Muda mrefu sana umepita tangu kushuhudia timu iliyokamilika kama hii PSG!

Hivi imekuwaje timu kongwe na kubwa za ulaya zimeruhusu PSG akusanye kikosi kilichokamilika namna hii!?

Huyo dogo Neves ni namba sita CHAFU kwelikweli, Vitinha kiungo ya mpira inapapasa mali kama imelaaniwa, Fabian Luiz kiungo yenye jicho la tatu, inakuwaje unaruhusu mtu atengeneze midfield iliyokamilika namna hii?

Fullbacks zao ni moto, wings ni balaa. Goalkeeper, JINI.

Eeeh bwana eeeh, sioni timu ya kuwazuia hawa jamaa. Tukishangaa UEFA wanaweza kuitia kwapani kwa mara nyingine.
Ilipofika January 2025 mifumo ya Luis Enrique ilkuwa imekaa sawa. Wakaanza kuubonda in style and fashion wakikutana na timu za Ulaya.

UEFA walistahili na hata hili kombe la dunia wanastahili pia vinginevyo Chelsea wajitahidi kuvuja jasho sana uwanjani. Jana Madrid alifanywa mbovu kupita maelezo. Ile energy na jinsi wanavyooverload eneo pinzani wakishambulia ni hatari sana.
 
Udambwi udambwi utakuwa mwingi sana

Wakimkaba Yamal kule kuna Raphinha, Ferran au Lewy

Dimba la kati kati kuna nyungu nyungu Pedri
​
Hamna kitu hapo. Hiyo kwa PSG ni sawa na vijana wa Mangungu tu mbele ya Vijana wa Hersi.

PSG wamekamilika. Chelsea wasiingize timu kwenye fainali kwani watapigika balaa.
 
Muda mrefu sana umepita tangu kushuhudia timu iliyokamilika kama hii PSG!

Hivi imekuwaje timu kongwe na kubwa za ulaya zimeruhusu PSG akusanye kikosi kilichokamilika namna hii!?

Huyo dogo Neves ni namba sita CHAFU kwelikweli, Vitinha kiungo ya mpira inapapasa mali kama imelaaniwa, Fabian Luiz kiungo yenye jicho la tatu, inakuwaje unaruhusu mtu atengeneze midfield iliyokamilika namna hii?

Fullbacks zao ni moto, wings ni balaa. Goalkeeper, JINI.

Eeeh bwana eeeh, sioni timu ya kuwazuia hawa jamaa. Tukishangaa UEFA wanaweza kuitia kwapani kwa mara nyingine.
Kwa sasa Ulaya ni PSgG na Bacca basi.
 
Hao PSG wako vizuri Sana.
Wapinzani ambao waliwasumbua ni Liverpool tu.
Ngoja tuone UCL msimu ujao.
 
Hao PSG wako vizuri Sana.
Wapinzani ambao waliwasumbua ni Liverpool tu.
Ngoja tuone UCL msimu ujao.
Kweli japo na wao Liverpool walichofaulu ni kupunguza magoli ya kufungwa tu ila kama ball PSG waliubonda sana games zote
 
Back
Top Bottom