matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 9,514
- 23,523
Ni kweli OR may be coincidence... lakini je, kuwa makao makuu ya nchi kumeanza leo?Kule ni makao makuu ya nchi Ila wangekuwa Malawi tungehitimisha Hivyo ulivyosema.
Kwa akli yake mbovu anaamini hivyo. Eti Tsunami haikutupata, kimbunga na Ebola hatukupata itakuwa haka kakorona? Yaani anaona watz ni wateule wa Mungu na hakuna baya ambalo linaweza kutupata. Anafikiri huko kote ambako watu wanateketea kwa kasi hawamjui Mungu? Au anafikiri Mungu anaishi Tz tu?Kulingana na Makonda jana, Watanzania Mungu anatupenda sana hawezi kufa mtu.
Wakati huo huo serikali na Rais wamehama Dar na wako Dodoma.
ndio maana Rais akaenda kujificha kwenye mawe Dodoma
Hivi mnaamini kabisa kwamba amekimbia Covid-19?Halafu yeye kaenda kujificha Dodoma kukwepa Corona!
Mtu ambae alikuwa haelewi kuwa Corona kishaingia Tanzania, hiyo atakuwa poyoyo wa mwisho.
Corona hayupo Dar Tu, Corona yupo Tanzania nzima na hata Dodoma yupo.
Dodoma serikali haikuhamia leo wala jana. Ni poyoyo tu asiyeelewa kuwa serikali ilishahamia Dodoma siku nyingi.
Kila mtu anatakiwa achukuwe hatua za salama za kujilinda yeye na wengine. Msingoje serikali iwafanyie kila kitu. Serikali yenyewe ni binaadam kama sisi na wao pia hawapo salama kwa corona.
Tusiwe wajinga.
Na hata hivyo, Corona ingeanzia kigoma Kwa mfano, Kwa maoni ya mtoa mada angelisema Kwa nini viongozi wasihamie huko!!!Hivi mnaamini kabisa kwamba amekimbia Covid-19?
Kwani kabla ya mlipuko wa huu ugonjwa hawakuwa wanaenda Dodoma?
Kwahiyo Covid-19 haipo Dodoma au haitafika Dodoma?
Acheni propaganda za ajabu!
Kama Wachina na teknolojia waliyo nayo wali introduce Lockdown na bado 3200+ wakafa....seuze Tanzania and other African countries??Bila lockdown haponi mtu.