Imetosha Rais Samia, rudi Nyumbani sasa

Imetosha Rais Samia, rudi Nyumbani sasa

Sipingi umuhimu wa safari ya Royal Tour Nchini Marekani, natambua faida za kimsingi za safari hiyo.

Mhe Rais tangu uondoke ni takribani wiki moja na ushehee sasa.

Tumeona msafara ulioambatana nao ukijumlisha na gharama za wasaidizi wako wa karibu, niseme imetosha Mhe. Rais rudi nyumbani sasa. Shughuli ya muhimu iliyokupeleka tayari imekamimilika. Shughuli ndogo ndogo kama za kutembelea viwanda vya viwatilifu hazina msingi wa kukufanya kuendelea kuwepo US.

Mhe. Rais imetosha. Unafanya mengi mema na mazuri wacha hili la kuoverstay US lisikuchafulie kwa wanaokupinga. Itoshe kusema imetosha.
Leo amekutana na baba yake na Rihanna, maskini Tanzania yangu!
 
Kapiga picha na baba yake Rihanna alafu mitandao na media wanaichapisha kama sifa! Kama Rais wetu kapata bahati ya mtende [emoji848]
 
ana bahati amekua rais kwenye nchi ya makobe,,,,,,maeneo kama Gabon huko angekuta ikulu ina watu wengine,,,,vyombo vyake vyote vipo nje
 
Mama alivyosema jipimie , nikakumbuka sekondari siku ya wali na nyama watu walikuwa wanakuja mess na vindoo vya lita 5 kujaza full hajali kuwa kuna wenzake wanaweza kukosa , sasa watu wa aina hio wakija kupata cheo Kwenye Ofisi ya umma inakuwaje ??

Shule niliyosoma alikuwepo prof mkumbo yeye akiwa mwenyekiti wa dormitory.
 
Sipingi umuhimu wa safari ya Royal Tour Nchini Marekani, natambua faida za kimsingi za safari hiyo.

Mhe Rais tangu uondoke ni takribani wiki moja na ushehee sasa.

Tumeona msafara ulioambatana nao ukijumlisha na gharama za wasaidizi wako wa karibu, niseme imetosha Mhe. Rais rudi nyumbani sasa. Shughuli ya muhimu iliyokupeleka tayari imekamimilika. Shughuli ndogo ndogo kama za kutembelea viwanda vya viwatilifu hazina msingi wa kukufanya kuendelea kuwepo US.

Mhe. Rais imetosha. Unafanya mengi mema na mazuri wacha hili la kuoverstay US lisikuchafulie kwa wanaokupinga. Itoshe kusema imetosha.
Wiki moja haijafika
 
Nadhani watanzania wanaoishi NY kama kuna wanazi wa siasa za Tanzania wanaokutana na hao watu private watakwambia kufuru ya msafara halisi na posho zao.

Sikia tu raisi anapoondoka airport unamuona pekee yake, ila mijitu iliyotangulia mbele yake kutoka kitengo cha raisi inaweza fika ata 50.

Na kwenye hizi ziara za matukio mengine ambazo zina wizara na taasisi mbalimbali sijui fedha, biashara, afya na watu wa mbugani huko mpaka siku uone wakiwa nje ya nchi kama ujawahi kuwaona ndio utaelewa kwanini Magufuli alizipiga marufuku hizi trip.
Ok tuseme uko sahihi, alipinga hizo ziara lakini alikuwa anaua raia wake. Je kipi ni kabaya kati ya ziara na uuaji wa raia wako kisa tu kakupinga?
 
Yeah, kwani kafika hapo kwa kushindana na kushindanishwa? Maisha ni awkward namna hiyo kwamba mnaweza jikuta mnaongozwa na mtu wa ajabu ajabu.
This is very true, ndiyo maana tukajikuta tunaongozwa na mtu kama Jiwe
 
It's very disturbing, hivi unaondokaje nchi yako ukitembelea nchi nyingine for days? I'll iweje...safari ya kikazi, hata kama ni hiyo tour, not more than 2days umerudi kwenye majukumu yako.

The real image of a normal Tanzanian inaonekana dhahiri hapa, tunapenda "kupumzika na kutembelea"!

Shame!
Ndiyo maana bwana yule aliyetuheshimisha alisema" HAPA KAZI TU" asiyefanya kazi na asile. R.I.P JPM
 
Ok tuseme uko sahihi, alipinga hizo ziara lakini alikuwa anaua raia wake. Je kipi ni kabaya kati ya ziara na uuaji wa raia wako kisa tu kakupinga?

Ata wewe unajua hilo swala ni la uongo vifo vilishatolewa maelezo na video zipo za watu waliokamatwa kwa ubebaji haramu.

Halafu mada inazungumzia ‘bi tozo’ kugeuka kiguu na njia kwa shughuli zisizo na lazima.

Kumbuka wazungu ni mabepari kweli kama ziara sio ya mwaliko wao elewa utalindwa kama raisi hilo nijukumu lao kukupa ulinzi. Lakini ukirudi wanakuletea bill ya gharama za ulinzi wao NYPD na LAPD hawana budget ya kumlinda raisi wa Tanzania kwa sababu anataka kuzurura tu marekani; hizo hela mtatoa walipa kodi jumlisha na za walinzi wake aliotoka nao Tanzania.
 
Back
Top Bottom