#COVID19 IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura

#COVID19 IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura

Mi sijakasirika,ye angeleta hoja tujadili,lakini kaanza kunitukana..rudia posti juu.. dawa ya moto ni moto,mbona sijakutukana wewe,nikamtukana yeye
Lkn mbona lipo wazi km wakati wa jiwe deni pia liliongezeka..
We sema tu hutaki aseme hvo manake sijaelewa hapo unachopinga nini?deni kupanda au hzo takwimu zake!![emoji848]
 
Nimekutana na habari hii ikanishtua sana!

Kwamba Kutoa takwimu tu za ugonjwa wa Corona IMF wanatoa such amount of money? Vipi kwa wanao accept Covid-19 vaccines?

Wajuzi wa mambo watusaidie hii imekaaje? Je, huu ndo utimilifu wa yanayosemwa na watu juu ya ugonjwa huu? Nini hasa kipo nyuma yake hadi IMF waseme hivyo? Ni kwa bahati mbaya au planned?

Anyway goja tupate maoni toka kwa wadau wa humu jamvini!
View attachment 1814143
 
JPM akifufuka Leo akakutana na hii mikopo 😳
Mikopo yenye iko kwa sasa ni kwa ajili ya JPM kimya kimya akiwadanganya eti miradi "ni kwa pesa za ndani", watch your budget news uone ni kiasi kipi walikopa, na ujue hii ni serikali ya CCM, propaganda lazima., ukweli hauwezi kuwekwa wazi.
 
Kwani korona haipo!?

Sasa kama ipo mnaficha takwimu za nini?

Hakuna kuanza kuwaza mawazo hasi

Dunia inatuonya tuende nao sawa

Sisi sio kisiwa

Hilo fungu ni kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa korona

Kama unaficha takwimu kama mwendazake hupewi!
 
IMF have revealed that Tanzania tried to ask for emergency loan from them and they were denied the loan until they start publishing covid data.


View attachment 1813837

=======

READ: - IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura
AbleIndelibleBasilisk-size_restricted.gif
 
Tanzania inahitaji kuweka wazi data ya ueneaji kwa Covid-19 kabla ya kupata idhini ya mkopo wa dharura wa Dola 574 milioni kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa. Maamuzi hayo yanatokana hali ya kutojulikana kwa takwimu halisi za ugonjwa huo tangu Serikali ilipoacha kuziweka wazi Mei mwaka 2020 wakati utawala wa Rais John Magufuli...
Missing Shujaa wetu. Tumekuwa ombaomba tena. Naona tunakopeshwa kujenga mabarabara vijijini SI MBAYA JE NI PRIORITY YETU KAMA NCHI?

Haya sasa mwisho watamwambia na visivyowezekana.
 
Hii mikopo mikopo enzi za jiwe tulishasahau..huyu mama anatuzingua.

wewe ni bure na haujui haya mambo. Hela ya Standard gauge tumetoa wapi? hela ya reli SGR tumetoa wapi? Hela ya kuboresha elimu hadi viongoxi wakalamba matapishi kusema hakutakuwa na ubaguzi kwa watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni

Hujui kitu kaa kimya
 
Kwani hizi taarifa za deni la taifa kukua kwa kasi ya 4G mlikua mnaziona au hamzioni wenzetu. Kwasababu hauna taarifa nayo haimaanishi haipo. Kwahiyo wewe akili yako inakutuma awamu ya tano haikua ikukopa kwamba wanajenga kwa pesa za ndani.
Kama Marekani na Ufaransa wanakopaga, itakuwa hizi nchi zetu za Afrika? 😂 Ubaya wetu huingia pale tunapotumia mikopo vibaya na inakosa kuleta profits zozote kwa serikali au hata inakuwa nyingi na kusababisha nchi kuwa na deni ju ya deni, miaka na mikaka.

Once ufisadi utakomeshwa na kuwe na responsibility katika hela tunayopewa, wallahi nina hakika sahi, tungekuwa na maendeleo ya kufa mtu, mwendo wa 5G yaani, kama wenzetu wanaokula "good life" ughaibuni. ✌️
 
Back
Top Bottom