TRA waliipata wap private email ya Mbowe, kama siyo yeye aliitoa kama business contact. Nawashangaa hao wanaosema SSH kasema hili kaema lile. Ukweli ni kuwa yale ya SSH ni siasa na hayawezi kufanyiwa kazi nje ya sheria. Mbowe atalia, ataelekezwa TRA, au kumfurahisha atapigiwa mkuu wa TRA na kuambiwa amshughulike mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA. Mkuu atamuagiza aliye chini yakle kumshughulikia. Atayeshughulika atafanya kazi tena kwa uangalifu wa juu. Ataangalia sheria na atakokotoa na usijeona ajabu akakutwa anadaiwa zaidi. Rais hawezi kuwambia wamkate kodi kidogo kuliko sheria inavyosema. Ninyi ngojeni tu! Mnashangilia lakini TRA hawanyi kazi hewani. Wanatumia sheria. Kama kuna nafuu inatafutwa, pelekeni hoja bungeni ya kutuinga sheria ya kupunguza kodi. Kama sivyo, mtakuwa mnadanganywa tu.
Kuna kitu kimoja, watu wengi hawakielewi. Tanzania ina watu wa aina mbili au tatu. Kwanza kuna watu wa pwani. Pili kuna watu wa mjini. Tatu kuna watu wa vijijini. Watu wa pwani huwa wapole, na wajanja katika lugha/Kiswahili. Watu wa pwani hawana lugha ya kulazimisha, na anapoongea usiamini kila anachokisema. Kwa kifupi wana "diplomatic language". Katika kundi hili yupo Kikwete, Mwinyi, na sasa SSH. Watu wa vijini wana lugha ya nguvu na ya kulazimisha. Hawa hutoa maagizo. Katika hili tulikuwa na Nyerere na Magufuli. Wale wa mjni ambao wako katikati tulikuwa naye Mkapa. Saa hivi kuna watu hawajamuelewa SSH. Huyu ni mtu wa pwani na lugha yake ni ya kipwani. Anaposema kitu chunga saana kuchukuliya maana juu juu. She is diplomatic, and you might easily be taken for a ride. Matamshi yake yote, hayana maana ya maagizo. Anayesema haya yote akijuwa masharti yatazingatiwa, yaani sheria itachukuwa mkondo wake. Kwa hiyo furaha bila mabadiliko ya sheria ni kujipa furaha isiyokuwepo.