#COVID19 Ina maana muda wote huu Rais alikuwa hajachanjwa?

#COVID19 Ina maana muda wote huu Rais alikuwa hajachanjwa?

I doubt! Binafsi nahisi alichanjwa. Ila hiyo tarehe atachomwa placebo.
 
Chanjo ndio zimeingia sasa hivyo ndio muda wa kuchanjwa huu.
 
Asingeweza kuchanjwa kabla hizo chanjo hazijathibitishwa kwanza.
Wengi walishachanjwa zile za kutoka China....ila unajua korona ukiwa nayo tayari wakati unachanjwa,chanjo haisaidiii na lolote laweza tokea..............
 
Huelewi!

Ndiyo, chanjo ni hiari. Hakuna mtu anayewekewa mtutu wa bunduki kumlazimisha achanje.

Lakini pia, mtu inategemea na unafanya shughuli gani maishani mwako.

Waajiri wengi sasa hivi wanawataka waajiriwa wao wachanjwe. Ila hawakulazimishi.

Kama hulipendi hilo takwa lao, basi, acha kazi hapo, nenda kwingine.

Mimi nimechanja kwa sababu ya convenience. Kazi yangu inanisafirisha sana.

Chanjo yenyewe ni bure. Wala sijadhurika kwa namna yoyote ile.

Kwa hiyo siyo kwamba nimechanjwa kisa ninaogopa corona. Nimechanjwa kuepuka usumbufu tu maana nyumbani watoto lazima wale na waende shule!

Nikiacha kazi wewe utanilipia ada za watoto shule?
Sawa mkuu, mimi nimechanja pia. Sababu ya kwanza naamini Corona ipo, ila siiogopi. Sababu ya pili ni kama yako.
 
Niliwaza hivyo yesterday.

Na pia naona kabisa kuwa kitakachofanywa leo ni kiini macho yawezekana kabisa alichanjwa kwa uhuru hapo.

Ngoja tuone
 
Keshokutwa tarehe 28, mwezi huu wa Julai, tumeambiwa kuwa Rais Samia atachanjwa hapa Ikulu ya Dar es Salaam.

Serikali ndo itakuwa inazindua kampeni yake ya chanjo dhidi ya Corona!

Sasa nimewaza tu: ina maana muda wote huu tokea Rais Magufuli afariki, huyu Rais wetu mpya alikuwa hajachanjwa?

Na Pia kumbuka hata barakoa alikuwa havai. Alikuwa anapuyanga tu huku na huko bila chanjo wala tahadhari yoyote ile!

Mara yupo Kariakoo…mara Mbagara [Mbagala]…mara Morogoro…Mwanza…Zanzibar…Nairobi na kwingineko huko.

Kote huko alikuwa anahutubia umati.

Very reckless behavior!

Unless labda alikuwa tayari keshachanjwa na hiyo keshokutwa kutakuwepo na ‘maonyesho’ tu ya kuwa anachanjwa na atachanjwa na dawa feki.

Otherwise, how does one explain her unseriousness?
Wewe unaamini kwamba chanjo ndo inayomlinda mtu???? Mbona mmechanganywa sana na chanjo mpaka mmemsahau Mungu??? Kwa hiyo wewe kwenye nchi hii ya watu milion 60, ni rais tu ndiye umemuona kuwa hakupaswa kutembea bila chanjo??? Kwa hiyo hapo kariakoo wote wamechanjwa????, chanjo isikuondoe ufahamu mpaka umemsahau Mungu kwamba ndo mlinzi wa kila kitu??? Tena nyie mnaongangania chanjo ,ndo wagonjwa wakubwa , hata mkiogopa kifo kifo kitakuja hata kwa ajali!! Acheni kujitoa ufahamu, Yesu muumba mbingu na nchi ndiye mlinzi wetu, tuliomo ndani ya Yesu hatutishwi na corona wala sijui barakoa!!
 
Tulihimizwa kusherekea kuondoka kwa corona kwenye kila kona ya nchi. Ilivyofika mwishoni mwa mei 2020, msimamo wa serikali ni kuwa corona ilitokomezwa, ndio maana viongozi wote wa serikali waliacha kuvaa barakoa na kufuata miongozo mingine ya wataalamu wa afya.

Akili za wapi hizo, unaambiwa imeisha nawe unakubali!!!! Kwakuwa ni serikali baas hukutaka kuhoji 😂 Sema haikumpata mmoja wenu katika el family ndio maana. Niulize mimi
 
Akili za wapi hizo, unaambiwa imeisha nawe unakubali!!!! Kwakuwa ni serikali baas hukutaka kuhoji 😂 Sema haikumpata mmoja wenu katika el family ndio maana. Niulize mimi
Mkuu naongelea "offical status" ya corona katika nchi, huo ndio ulikuwa msimamo wa nchi na ndio maana viongozi wote waliacha kuchukua tahadhari.

tmimi wakati wanatoa takwimu kwenye makoti ya suti na kujisifu imekwisha niliumwa hadi kufikia hatua ya kutokuwa na uhakika kama naweza kumaliza wiki, msimamo wangu ulikuwa ni kupinga propaganda zilizokuwa zinaenezwa na wanasiasa kusema ugonjwa haupo.
 
Pamoja mkuu
 
Kwa nini ulihamasishwa nyungu kama corona iliisha? Iko tofauti kubwa ya corona kwisha na corona kudhibitiwa. Hili la mwisho ndio sahihi corona ilidhibitiwa kulinganisha na kwengine ulimwenguni.

Kumbuka tulitangaziwa na hao wanaotupa chanjo leo kwamba tusipo chanjwa tutapukutika kama kuku mdondo. Wakaona ola tumeidhibiti. Wakabaki na aibu yao

Kwa vile tumekubali watuletee chanjo sitashangaa kama kauli ya kufa na kuzagaa mtaani ikatiamilika.!! Nasema hivyo kwa vile najua hatuwezi kwa kutumia mfumo wa afya ulioko kushindana na madhara ya yatokanayo na huko kuchanjwa hii chanjo yenye sintofahamu nyingi. Nawaonea huruma sana Watanzania wale hasa wa huko vijijini waliko wengi mno.

Hebu niambie mimi ni mlinzi wa Rais inner circle hiari yangu sitaki kuchwanjwa. Ninaye mlinda amechanjwa hivyo anaambukiza corona.
Sasa nitakuwa na mlinda Rais , ndiyo kazi na huku nikijilinda dhidi ya corona inayotoka kwa ninaye mlinda. Kweli hatuoni kuwa tayari hili ni tatizo. Vinginevyo walinzi nao wachanje kwa lazima hamna kitu kama hiari tena hapo.
 
Back
Top Bottom