Inadaiwa Klabu ya Simba imezuiliwa kuingia Mkapa kufanya mazoezi kuelekea Kariakoo dabi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Ubaya Ubwela umewageukia!

Kwa mjibu wa Watangazaji wa EFm Inadaiwa Klabu ya Simba imezuiliwa kuingia Mkapa kufanya mazoezi kuelekea Kariakoo dabi


Tazama video hii ya tukio husika


Mwendelezo:

Kikosi cha Simba, kimeondoka katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kurejea kambini baada ya kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi.

Simba SC walikuwepo uwanjani tangu saa moja ila imeshindikana wao kufanya mazoezi baada ya kuzuiwa.
IMG_3420.jpeg
IMG_3421.jpeg


Kuhusu SHERIA

Sheria za soka, hasa chini ya FIFA na mashirikisho kama CAF na UEFA, zinaeleza haki za timu mgeni kuhusu matumizi ya uwanja kabla ya mechi. Kwa kawaida, masharti haya yanahusiana na mazoezi ya mwisho na kukagua uwanja.

Masharti Muhimu kwa Timu Mgeni:

1. Siku Moja Kabla ya Mechi: Timu mgeni kwa kawaida inaruhusiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja rasmi wa mechi siku moja kabla ya mchezo.

2. Muda wa Mazoezi: Kuna kikomo cha muda wa kutumia uwanja, mara nyingi kati ya dakika 60 hadi 90, kulinda hali ya nyasi.

3. Hali Mbaya ya Uwanja: Kama uwanja uko kwenye hali mbaya (mfano, mvua nyingi), mwenyeji anaweza kuzuia mazoezi hapo ili kuulinda, lakini timu mgeni inapaswa kuruhusiwa kuukagua.
photo-output.jpeg


Adhabu

IMG_3430.jpeg


Pia, Soma
 
Unaweza kukuta hiyo ndiyo fursa ya Simba kurogwa hapo hapo maana vyura wamezunguka basi la Simba
 
Tuko uwanja wa Taifa tunataka kufanya mazoezi ya mwisho uwanjani, tumezuiwa.Tafadhalini jamani
 
Sizani kama mechi za watani kama zina utaratibu huu na sijawahi kuona hiki kitu kwenye mechi watani hata moja sijawahi tokea nianze kufuatilia mpira. Mara nyingi wanyumbani ndiye anaye kabidhiwa uwanja.
 
Back
Top Bottom