Kwa mjibu wa Watangazaji wa EFm Inadaiwa Klabu ya Simba imezuiliwa kuingia Mkapa kufanya mazoezi kuelekea Kariakoo dabi
Your browser is not able to display this video.
Tazama video hii ya tukio husika
Your browser is not able to display this video.
Mwendelezo:
Kikosi cha Simba, kimeondoka katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kurejea kambini baada ya kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi.
Your browser is not able to display this video.
Simba SC walikuwepo uwanjani tangu saa moja ila imeshindikana wao kufanya mazoezi baada ya kuzuiwa.
Kuhusu SHERIA
Sheria za soka, hasa chini ya FIFA na mashirikisho kama CAF na UEFA, zinaeleza haki za timu mgeni kuhusu matumizi ya uwanja kabla ya mechi. Kwa kawaida, masharti haya yanahusiana na mazoezi ya mwisho na kukagua uwanja.
Masharti Muhimu kwa Timu Mgeni:
1. Siku Moja Kabla ya Mechi: Timu mgeni kwa kawaida inaruhusiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja rasmi wa mechi siku moja kabla ya mchezo.
2. Muda wa Mazoezi: Kuna kikomo cha muda wa kutumia uwanja, mara nyingi kati ya dakika 60 hadi 90, kulinda hali ya nyasi.
3. Hali Mbaya ya Uwanja: Kama uwanja uko kwenye hali mbaya (mfano, mvua nyingi), mwenyeji anaweza kuzuia mazoezi hapo ili kuulinda, lakini timu mgeni inapaswa kuruhusiwa kuukagua.
Kwa timu ngeni kutoka Nje ya Nchi au Mkoa mwingine sio uwanja unaotumia kila siku useme ww ni mgeni? Game iliyopita Yanga walienda Taifa kufanya mazoezi?
Kwa timu ngeni kutoka Nje ya Nchi au Mkoa mwingine sio uwanja unaotumia kila siku useme ww ni mgeni? Game iliyopita Yanga walienda Taifa kufanya mazoezi?
Sizani kama mechi za watani kama zina utaratibu huu na sijawahi kuona hiki kitu kwenye mechi watani hata moja sijawahi tokea nianze kufuatilia mpira. Mara nyingi wanyumbani ndiye anaye kabidhiwa uwanja.