Wakuu
Ubaya Ubwela umewageukia!
Kwa mjibu wa Watangazaji wa EFm Inadaiwa Klabu ya Simba imezuiliwa kuingia Mkapa kufanya mazoezi kuelekea Kariakoo dabi
View attachment 3262877
Tazama video hii ya tukio husika
View attachment 3262905
Mwendelezo:
Kikosi cha Simba, kimeondoka katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kurejea kambini baada ya kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi.
View attachment 3262951
Simba SC walikuwepo uwanjani tangu saa moja ila imeshindikana wao kufanya mazoezi baada ya kuzuiwa.
View attachment 3262928View attachment 3262929
Kuhusu SHERIA
Sheria za soka, hasa chini ya
FIFA na mashirikisho kama
CAF na
UEFA, zinaeleza haki za timu mgeni kuhusu matumizi ya uwanja kabla ya mechi. Kwa kawaida, masharti haya yanahusiana na mazoezi ya mwisho na kukagua uwanja.
Masharti Muhimu kwa Timu Mgeni:
1.
Siku Moja Kabla ya Mechi: Timu mgeni kwa kawaida inaruhusiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja rasmi wa mechi siku moja kabla ya mchezo.
2.
Muda wa Mazoezi: Kuna kikomo cha muda wa kutumia uwanja, mara nyingi kati ya dakika 60 hadi 90, kulinda hali ya nyasi.
3.
Hali Mbaya ya Uwanja: Kama uwanja uko kwenye hali mbaya (mfano, mvua nyingi), mwenyeji anaweza kuzuia mazoezi hapo ili kuulinda, lakini timu mgeni inapaswa kuruhusiwa kuukagua.
View attachment 3263101
Adhabu
View attachment 3263102
Pia, Soma