sayoo
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 5,280
- 7,930
Wabongo kwa mikwara kwenye keyboards hua hawajambo , ila uhalisia hua hakuna kabisa ,Leo wamepitisha matangazo jijini Mwanza kwamba kwanzia jumatatu hawataki kuona machinga yoyote mjini, lakini hatujui wanataka watuone wapi, wanaotangaza haya wao ni watumishi wa serikali wanatembelea magari, kipato chao ni serikalini,
sisi kipato chetu ni mtaani kwanini mtufukuze?
tukale nyumbani kwenu?
Tumesoma kwa gharama mmekataa kutuajiri tumejiajiri mnatufukuza
mnadai machinga hawalipi kodi kwani sisi tumewazuia kutudai kodi? mlikuja kuombatukakataa?
mnasema tunaziba njia mlishasikia gali imeshindwa kupita kisa machinga? kati ya katikati na mji na pembezoni mwa mji ni wapi ajali hutokea mara nyingi?
haiwezekani haiwezekani haiwezekani
jumatatu afe beki afe kipa heri nifie barabarani lakini sitakubali kunyanyasika bila sababu za msingi,
Jumatatu mkae kwa umakini Tuna jambo letu
Tumechoka upuuzi
Magufuli aliwaachia watanzania hofu na uoga tu