Inadaiwa marehemu Swalha alikuwa analazimisha talaka ili arudiane na mume wake wa zamani na siku ya tukio alienda nae kwenye tamasha la muziki

Inadaiwa marehemu Swalha alikuwa analazimisha talaka ili arudiane na mume wake wa zamani na siku ya tukio alienda nae kwenye tamasha la muziki

Wanawake ni watu wa ajabu sana. Mimi wa kwangu nilivyoona ananiletea vitimbwi vya kutoka jioni saa moja anarudi usiku saa tano Anakuta nimeshapikia watoto na kuwalisha na yeye anachukua chakula nilichopika anakula nikajua hapa tunapoelekea kutakuwa pabaya zaidi

Nikamuambia nimebadilishwa kituo changu cha kazi
Akaniuliza wapi? Nikamuambia sijajua nitakuambia nikishafika
Nikaweka nguo kwenye begi nikatupia kwenye gari yangu nikaondoka nikanunua simu ya nikamuelekeza mtoto wangu mkubwa akachukue kwenye duka flani hivi Ili niwe natuma pesa hapo via Airtel money
Mpaka Leo hii hapa
Nilim-block sikutaka hata kusikia sauti yake nikaenda nikapanga nyumba nikaanza maisha mapya
Nikawaelekeza watoto home wanakuja Kila week end wanakaa nawapeleka out wanafurahi jumatatu jumapili jioni nawarudisha shuleni
Ndio imeisha hivyo
Usiongeze tatizo juu ya tatizo. Wana laana hawa watu. Ametoka kwao masikini wa kutupwa amejimilikisha mjengo kirahisi kabisa. Na ndio wanavyofanya siku hizi akishaona mafanikio
Hakusumbui huyo mke wako hapo ulipohamia?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo umempa faida yeye maana lengo lake ni wewe umwache hilo kafanikiwa. Shida ya jamiiforum kila mtu ana gari isipokuwa mm tu ebu onyesha kadi ya hilo gari unalosema
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji91][emoji91][emoji91][emoji16][emoji16][emoji16]

Mkuu gari ni kitu cha kawaida daah[emoji1787][emoji1787]
 
Story zote fake, mara alimjengea nyumba na magari? yeye hana gari anaomba lift kwa mkewe. Mara alimsomesha mara alikuwa muuza bar. Mara alimuomba ruhusa mumewe anatoka akamruhusu ila alichelewa kurudi, mwanammke gani akamruhusu mkewe atoke usiku peke yake. Hizi story bado hazijakaa sawa
Fake story mpaka vichekesho tunaoujua ukweli acha tucheke tu, kikubwa huyo Said alikuwa mgonjwa wa akili na hela alikuwa nazo zamani kipindi cha JPM alifirisika ndo akaanza upya alipoanza kupata pesa akamuweka pembeni mke mkubwa ndo kwenda kumuoa huyo bi mdogo ila huyo bi mdogo alimkuta tayari na maisha yake mazuri kiasi aliyotoka nayo kwa mume wa Kwanza na mume wa Kwanza ndo alimuachisha shule na kumjenga kiuchumi tatizo likawa mtoto kitu kilichofanya aachike na kuanza kuishi maisha ya kihuni na starehe na huyo Said kamuoa akijua tabia zake.
 
Habari za ndani kabisa zinasema:

1. Marehemu kabla ya kuolewa na SAID alikuwa ameolewa na jamaa maeneo ya Kirumba Mwanza kisha wakaachana. Sababu ya kuachana inasemekana ni ex mume wake kutokuwa na pesa

2. Marehemu akaolewa na SAID na inasemekana alifuata pesa kwa SAID

3. Said alimjengea marehemu nyumba tatu na gari 2 plus kumfungulia biashara ya saluni.

4. Baada ya kupata mali marehemu akaanza vituko kwa Said kwa sababu inasemekana hakuwa akimpenda kwa dhati Said na kwamba kwa Said alifuata hela tu, so akawa anafanya vituko ili Said atoe talaka ili marehemu arudiane na ex wake but Said akawa anagoma kutoa talaka licha ya vituko.

5. Siku ya tukio kama mlivyo sikia wengi kulikuwa na : missed call 42, marehemu inasemekana alipotoka out alikuwa na ex husband wake.

CHANZO: AFRICANDADAZ BLOG

Pia soma >
Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI
Uongo; wameoana Dec.30, 2021

Kwa hiyo ndani ya miezi mi 5 ajengwe nyumba 3, afunguliwe biashara ya salon, na bado aombe talaka ndani ya kipindi hicho hicho kifupi?
 
Wakati mwingine mwanaume anapata mwenye mapenzi ya kweli lakini wanakuja kuwaumiza . Mimi aliyekuwa mume wangu nilimpenda kwa dhati pamoja na kuwa alikuwa ana maisha ya chini. Tukafunga ndoa tukaishi vizuri tu miaka 3. Mwaka wa 4 akadanyika na mchepuko akawa anachelewa kurudi, mara apotee mwezi anakuambia yuko msata kwenye shughuli zake. Mbaya zaidi akadanganywa na kuniibia gari langu akabadilisha kadi ya gari na kwenda kuiuza mimi sina hata habari maana gari alikuwa anatumia yeye. Vituko vikawa vituko. Wala sikutaka ugomvi na yeye na huyo mwanamke, nikawaita familia pande 2 nikawaambia naondoka naenda kuanza maisha mapya. Nyumba naiacha na gari yangu ndio imeshauzwa hivyo wamenunua gari nyingine. Mungu alienipa mali hizi atanipa nyingine. Nikaenda zangu kupanga na kuanzz upya. Baada ya mimi kuondoka alipangisha nyumba akahamia huko na mchepuko. Baada ya miezi 3 wakagombana vibaya na mchepuko sababu hela zimeisha na michongo ya hela nayo imekata. Sasa hivi yupo tu maisha yamempiga . Sikutaka kurudiana naye tena maana niliona atazidi kuniharibia maisha.
Pole shost but mbona kama wewe ndo ulioa?[emoji849][emoji849][emoji849][emoji848]
 
Kwahio alitaka aachike aondoke na mali kirahisi like that??

Hapo mabinti wapenda hela bila kuzifanyia kazi mjifunze kwa kweli
Tafuteni zenu jmn

Ningekua mwanaume nisingekuua ila ningechukua kila kitu changu
Hela ngumu jmn nyiee
 
Fake story mpaka vichekesho tunaoujua ukweli acha tucheke tu, kikubwa huyo Said alikuwa mgonjwa wa akili na hela alikuwa nazo zamani kipindi cha JPM alifirisika ndo akaanza upya alipoanza kupata pesa akamuweka pembeni mke mkubwa ndo kwenda kumuoa huyo bi mdogo ila huyo bi mdogo alimkuta tayari na maisha yake mazuri kiasi aliyotoka nayo kwa mume wa Kwanza na mume wa Kwanza ndo alimuachisha shule na kumjenga kiuchumi tatizo likawa mtoto kitu kilichofanya aachike na kuanza kuishi maisha ya kihuni na starehe na huyo Said kamuoa akijua tabia zake.
Kwahiyo Swalha alikuwa well off kiuchumi?

Huyo x mme wake mbona tunaambiwa ni kapuku humu?

Ni kweli kampa nyumba tatu magari na saluni?
 
Na wewe mtu humpendi, kwa nini unaingia naye kwenye ndoa halafu baadaye unataka kuishi maisha yako kama vile uko single?

Kwamba alifuata pesa….

Ni pesa kiasi gani hizo ambazo yeye mwenyewe hakuwa na uwezo wa kuzitengeneza?

Mi naona wote walikutana wajinga wajinga tu.
Na ujinga mkubwa ulijidhiirisha pale alimpomjengea nyumba "mke" na kumkabidhi tena tatu na biashara ya saloon On time
 
Maslay qn sijui y hawaridhiki

Cheap thinking

Basi walau angechepuka kwa siri sana asiachike tena
 
Kwahiyo Swalha alikuwa well off kiuchumi?

Huyo x mme wake mbona tunaambiwa ni kapuku humu?

Ni kweli kampa nyumba tatu magari na saluni?
Hakuwa kapuku ni maneno ya kujifurahisha tu, Swalha kilichomutoa kwa mume wa Kwanza ni kukosa mtoto na siyo umasikini, alafu huyo Said kamuoa akiwa na saluni yake kubwa tu na alikuwa na jina tayari kwa kufanya makeup, huyo Said alipomuoa hakutaka afanye tena hiyo kazi na alitaka wazunguke naye visiwani tu kitu kilichofanya wapambe wa Swalha kumshauri asiache biashara yake na ndo ugomvi wa ndoa yao ulipoanzia maana mwanaume alitaka mke atulie ndani tu au akubali kuzunguka naye visiwani Sasa mke akaanza kudai talaka Ili awe huru na kazi zake na starehe zake.
 
Umenikumbusha kitu, mimi huwa nikiona wife analeta dharau huwa naweka status picha nikiwa site na mtoto mkali tunapiga kazi, offcoz anashindwa kuniwashia kwa sababu anaona ni mazingira ya kazi ila kwa uzuri wa hizo pisi lazima ajiulize nina stahili kuletewa jeuri! Maana utakuta nimetoka hone kaninunia alafu anaona vibinti site vinanichekea. Basi hapo nitapetiwa petiwa wiki kadhaa tu baada ya muda anajisahau tena. Hawa viumbe wakijua hauna plan b watakunyanyasa sana.
Dawa ya mwanamke ni mwanamke mwenzake, sijui kwa nini wanaume tunashindwa ku-apply hii principle.......sijui ndo haya mambo ya ndoa ya mke mmoja walotuletea wazungu. Hiyo ni moja ya adhabu ambayo Mungu alitoa kwa mwanamke, kwamba atakuwa na wivu kwa mume wake. Mtu una pesa, mwanamke anazingua......unashindwa kutoka na mwanamke mwingine kweli? unashindwa kum-blackmail na kumwekea sanctions hadi akili imkae sawa? Mfano, mchukulie Kanye West, si anatoka na kifaa kingine na maisha yanaenda.........
 
Hakuwa kapuku ni maneno ya kujifurahisha tu, Swalha kilichomutoa kwa mume wa Kwanza ni kukosa mtoto na siyo umasikini, alafu huyo Said kamuoa akiwa na saluni yake kubwa tu na alikuwa na jina tayari kwa kufanya makeup, huyo Said alipomuoa hakutaka afanye tena hiyo kazi na alitaka wazunguke naye visiwani tu kitu kilichofanya wapambe wa Swalha kumshauri asiache biashara yake na ndo ugomvi wa ndoa yao ulipoanzia maana mwanaume alitaka mke atulie ndani tu au akubali kuzunguka naye visiwani Sasa mke akaanza kudai talaka Ili awe huru na kazi zake na starehe zake.
Makes sense
 
Back
Top Bottom