Mwenyezi Mungu atawaumbua tu watekaji watajulikana tu ,shetani hajawahi kumshinda Mungu .
THAMANI YAKO HUPIMWA KWA MSIBA WAKO
Nimeona kwenye Tv na kwenye mitandao ya kijamii namna maelfu ya watu waliojitokeza kuupokea na kuuaga mwili wa Dr. Reginald Mengi aliyeiaga dunia akiwa huko Dubai.
Wingi wa watu niliouona ndio ulionisukuma kuzama katika tafakari hii kuu;
Kumbe katika haya maisha yetu yote ya uhai hapa duniani pamoja na mambo mengi tunayofanya lipo jambo moja kuu tunalifanya pasipo kujitambua nalo ni KUWAANDAA WATU WATAKAO KUJA KUKUSINDIKIZA SIKU SAFARI YAKO YA MWISHO IKIFIKA? Ndio, kwa sababu idadi ya watu watakaokuja kukusindikiza siku hiyo ya mwisho itafanana na idadi halisi ya watu uliowahi kuwagusa katika maisha yao, itategemea vile ulivyoishi na ulifanya nini kwa watu hao pindi ulipokuwa mzima hapa duniani. Ndio maana wengine huzikwa na watu wachache ikiashiria aligusa watu wachache pia. Thamani ya msiba wako hutengenezwa ukiwa hai... Kifo cha Dr. Reginald Mengi kitufundishe na kutukumbusha kutengeneza thamani ya maisha yetu.
Kama uliwathamini watu katika uhai wako basi hata siku yako ya mwisho itakapofika, wakati huwezi kuona, huongei wala hupumui watu wale uliogusa maisha yao hujitokeza kuelezea wasifu wako. Watakumwagia sifa kem kem, watakuletea zawadi za kila aina, watachangishana mamilioni kwa mamilioni, watakuvika mavazi ya gharama, watakutembeza kwenye magari ya thamani huku wakiimba na kukulilia... Idadi yao itakuwa kubwa kuliko wakati wowote wa uhai wako. Watakuja hata wasiokujua ili mradi tu kama aliwahi kusikia jina lako.
Maisha ya hapa duniani ni mafupi sana hivyo tujifunze kuishi vema na watu ili siku yako itakapofika mwisho watu wale wajitokeze kwa idadi ile ile waje wakuimbie, wakulilie na mwisho wakusindikize na kukuhifadhi kwa heshima!
Ewe ndugu yangu uliyebahatika kusoma ujumbe huu unautumiaje muda wako katika kuwatayarisha watu wa kukusindikiza katika safari yako ya mwisho? Kumbuka thamani yako itapimwa kwa msiba wako!
Iko siku bashite na jiwe watajiuliza hayo hapo juu ila itakuwa wamechelewa badala ya kuliliwa watakuwa wanazomewa kwenye majeneza yao hadi kaburini.
KIBURI KIMEWAJAA, USHETANI UMEWAJAA, UMWAGAJI DAMU,UTESAJI NA JEURI YA MADARAKA.
ILA MAVUMBINI UTARUDI