Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Kila nikitazama kipindi cha the last door cha kenya natamani na sisi kungekuwa na vipindi kama hivi.Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum.
Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa hapo kabla. Hivi karibuni jambo hilo litawekwa wazi.
Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia na kuujadili utawala wa hayati John Magufuli. Imefahamika kuwa yapo mambo kadhaa yasiyo ya utu yalifanyika huku yakiwa na baraka za hayati John Magufuli tena kwa maelekezo maalum.
Wekeni masikio wazi siku chache zijazo mtasikia la mgambo.
Ila askari wa kenya ni mafia. Ile wiki walionyesha documentary ya kikosi maalum walivyokuwa wanaua watu wanachukua mili yao wanaimwagia acid na kuitupa mtoni ikiwa kwa magunia.
Jana wameonyesha documentary ya askari walivyomuua mtu anayewashitaki, ndugu yake na mwanasheria aliyekuwa ana simamia kesi yake kisha wakaitupa miili mtoni ikiwa kwenye magunia.