Tetesi: Inaelezwa Ali Kamwe kafungiwa miaka 2, Ahmed Ally anusurika na rungu la TFF

Tetesi: Inaelezwa Ali Kamwe kafungiwa miaka 2, Ahmed Ally anusurika na rungu la TFF

TFF wanajua Kolo ni nani, Utopolo, Nyuki wa Tabora, Gongo wazi,Mbumbumbu,Lambalamba..

Mahakamani unaweza mtukana John na ukaachiwa kwasababu hati ya mashtaka imeandikwa John Magufuli.

TFF hawafanyi kazi hivyo.
Okay kwani Kolo FC kwenye NBC premier league wanashika nafasi ya ngapi na uwanja wao wa nyumbani ni upi?

Mpira bila utani hauna maana na sizani hata hili jukwaa la Sports kama lingekuwepo, wanachofanya ni kujikaanga wenyewe kama nguruwe.
 
Kesi yao iliahirishwa na kusogezwa mbele, Waufukweni acha kuleta stori za vijiweni na kutoka kwa wachambuzi uchwara,nilikuwa nakukubali sana mkuu,ila ukiendelea na stori za vijiweni utaonekana wa hovyo na utapuuzwa. Badilika mkuu.
Iliahilishwa wakati walisikilizwa jana kutoa ushahidi na kujitetea?
 
Hao watoto bado hawajielewi. Wanashindwa kuchunga midomo yao na wanasahau kuwa wapo kazini.
 
Kwa hiyo kilicho mponza Kamwe ni hiki?
View attachment 3260907
Inamaana kwenye NBC league kuna timu inaitwa Kolo.......
Nawaambia humu kila siku kuwa mna utetezi wa kitoto sana. Mnadhani mnadili na watoto wadogo kumbe watu wanawaangalia tu.

Sasa kujitetea kwa kuhoji kolo ni nani na wao wakimuuliza kolo ni nani atajibuje? Kumbuka hawa wasemaji walionywa waache kuwa comedians na wafanye kazi zao kwa weledi kwa hiyo kusema umejitungia tu timu na kupost vichekesho wakati yoyote mwenye akili timamu anajua unachokiongelea ni kuwakosea heshima wanaokuhoji.
 
Mbona easy "Kolo FC ni timu yetu ya mtaani......".

Maana timu zote anazo zisimamia TFF zimesajiliwa na kutambulika na TFF. Sasa Kolo FC imesajiliwa wapi? Kwenye ligi inashika nafasi ya ngapi? Uwanja wake upo wapi?.

Au labda uniambie wewe Kolo FC inashika nafasi ya ngapi kwenye msimamo wa ligi.
 
Ally Kamwe kufungiwa TFF sisi wanasimba inatuhusu nini? Hamuoni kuwa kuna mpango wa kutuzubaisha ili jumamosi watuue halaf Ally Kamwe asisimamishwe tutakuwa tumepata nn

Kamwe akiadhibiwa sisi anatuhusu nn wanasimba, Yanga mm kwangu ni adui tu sina urafiki naye

Achaneni na habari za Ally Kamwe, atajua mwenyewe na balaa lake
 
Sasa habari kama siyo ya kweli inakutoaje mchezoni ? Au ndo maneno ya kujifariji ili ukifungwa upate chakulalamika
 
Mbona easy "Kolo FC ni timu yetu ya mtaani......".

Maana timu zote anazo zisimamia TFF zimesajiliwa na kutambulika na TFF. Sasa Kolo FC imesajiliwa wapi? Kwenye ligi inashika nafasi ya ngapi? Uwanja wake upo wapi?.

Au labda uniambie wewe Kolo FC inashika nafasi ya ngapi kwenye msimamo wa ligi.
Badala ya kumsaidia huyo dogo wenu mnazidi kumpoteza kwa kumjaza maujinga.

Atoe ushahidi ni mtaa gani hiyo timu ipo atupeleke halafu atoe ushahidi wa madai yake kuwa hiyo timu ya mtaani imependelewa mechi 10 na upuuzi mwingine alioutapika katika post hiyo.

Kumbuka unadili na mamlaka ya soka ambayo kuanzia ligi kuu hadi ligi za mchangani kote zipo kwenye mamlaka yake.

Mkiacha utoto mtaacha kuongea hovyo na kudhani mnadili na watoto wadogo wasiojielewa.
 
Mtaa mbona mtaani kwetu ipo timu Kolo FC halafu tokea lini timu za mtaani zikawa na usajili? Huku mtaani timu asubuhi inaweza itwa mbinde FC jioni inaitwa Kolo FC.

Mamlaka zote hazideal na majina ya utani wasiyo ya sajili, bali wanadeal majina waliyo ya sajili.
 
Mshabiki anatolewa kwenye mchezo ili iweje? Anacheza? Ni kocha? Nashindwaga kuelewa hizi hoja za kutolewa kwenye mchezo.

Lakini nina mashaka huenda hizi tetesi za Kamwe kufungiwa hazina ukweli, ila zimetengenezwa ili kuwafanya TFF wasite kumfungia. Huenda amekutwa na hatia lakini bado hawajaamua kuhusu adhabu, sasa Kamwe amewatumia watu kutengeneza habari feki ili iibue ukosoaji na huruma na kuwafanya TFF wasitoe adhabu yoyote ya kumfungia.

Na naona wamefanikiwa. Atapigwa faini. Hata hivyo sijaona kosa la kumfungia. Faini na onyo vinatosha.
 
Mtaa mbona mtaani kwetu ipo timu Kolo FC halafu tokea lini timu za mtaani zikawa na usajili? Huku mtaani timu asubuhi inaweza itwa mbinde FC jioni inaitwa Kolo FC.

Mamlaka zote hazideal na majina ya utani wasiyo ya sajili, bali wanadeal majina waliyo ya sajili.
Kama Kamwe amejitetea hivi, si maajabu kashindwa kesi.
 
Back
Top Bottom