Inakuwaje Kitambaa Cheupe Sinza kunafurika kila siku?

Hamna hiko kitu we mzee baba
 
Kweli?? Mmmh basi atare
 
Acha mawazo ya kijinga. Hamna cha kafara wala nini. Nani ana muda mchafu huo, vitu sikuhizi ni customer care nzuri.
Naungana na wewe. Kuna siku nilitoka kumsubiri mgeni wangu Urafiki pale pana bar ya Kilimanjaro.
Sasa wakati narudi mida ya saa saba usiku nikakuta pale Manzese darajani kwa Mkwere pamechangamka sana, ikabidi nipitie.
Nilivyofika yaani pale nje tu wanakupokea vizuri, anakupeleka kwenye siti ambayo ni tupu na anaivuta kabisa ili mheshimiwa mnywaji ukae, anakukaribisha sana kisha anakuuliza unakunywa kinywaji gani!
Nilipanga kunywa bia 2 lakini nikakesha hadi kumi na moja.
 
Kuna chimbo moja liko Himo njia panda sikumbuki jina ila misiba yote ya Kaskazini lazima ikutane hapo night then asubuhi kila mtu anasepa kivyake.Watu wanakula bia Mpaka maiti zinashangaa yaani mwenye ile chimbo kawini.
 
Dar viwanja huwa vinakuja na kuondoka ila Elements iko kwenye peak miaka yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…