Miujiza ni kitu kinachowezekana Kwa wenye haki na wasio haki mkuu....Kwa maana Mungu ananamna yake ya kukutana na watu....
Mimi kipindi muhuni muhuni tu nimewahi kuwaombea wanafunzi hadi wakadondoka na kutapika vitu, pia mimi nimewahi fanya maombi ya uhitaji nikapata milioni 1 Kwa njia ya ajabu,
Pia mimi nimewahi oneshwa kuhusu ukimwi basi nikaomba sana Mungu aniepushe na ugonjwa huo japo nilisali juu juu tu nikawa sielewi kwanini lakini week mbili nzima nilikuwa nawaza ukimwi na kukutana na makala za ukimwi... guess what baada ya week hizo 2 nikakaa week 1, my favourite girl niligundua anavirusi vya ukimwi, imagine nilidumu nae miaka 2, imagine nilizini nae kavu...
Lakini nipo salama mkuu, na sijui nimepitaje pitaje.