Ni wazo tu nimepata kwamba mwanadamu ambaye inasadikika kutoka kwenye maandiko kwamba alipewa ukuu na umiliki juu ya vyote vilivyopo duniani
Kipindi anapewa huo umiliki kulikuwapo na shetani ambaye kwa logic tu ya kawaida yuko most powerful 1000000000% than a human
Sio kiakili wala nguvu tu za kufanya mambo
Nawale mapepo zake ambao wapo wenye nguvu hata kumzidi sasa hapo utawala unakuwaje?
Baasi huko tumefikiria mbali hata simba au tembo tunaowatawala wanatuuwa sometimes why isiwe kama mfalme akutanapo na anayemtawala iwe anamjua hamjui lzm anyenyekeee chini
Ninashuhuda ya maisha yangu binafsi,
Nikiwa mdogo wa miaka 7
Nilitekwa na watu katili nikiwa shule nikafungwa mikono na miguu, huku nimeshindiliwa mdomoni vipande vya magodoro na vitambaa vikuu kuu
Lengo lilikuwa kunipeleka nitolewe Kafara mirerani.
Kwa muujiza wa Mungu nilinusurika kimaajabu na kuanza kutambaa kuelekea Polini kwa siku kadhaa,
Ninatambaa kutumia makalio, Nikawanapishana na majoka makubwa manene mpaka leo nikiyakumbuka natetemeka, cha ajabu Sikuwa na hofu na yale majoka hata kidogo, zaidi nilikuwa na hofu na wale watu wasije kuniona wakaniua.
Hapo ndipo nikajua kuwa majoka huwa yanaweza kusimamia mkia na kupigana, huku wakiwa hawana kabisa time na mimi, wakati walikuwa wanauwezo wa kunimeza na wasinishibe[emoji15]
Wanyama wakali walikuwa wananipita wananitazama kana. kwamba wananishangaa wakiendelea na mambo yao mengine.
Mpaka nilipoishiwa nguvu kwa njaa na kiu ya maji nikapoteza fahamu nilipozinduka nikajikuta niko kwa Wamaasai wameshanifungua kamba na kunitoa Magodoro mdomoni.
Baada ya kunitibia majeraha makubwa nilokuwa nayo kwa muda mrefu, Ndipo walinieleza kwa kushangazwa kunikuta Kule mbugani Manyara nikiwa sijazuriwa na wanyama zaidi ya Ruba waliokuwa wamenijaa kwa kuwa sehemu nilipopotezea fahamu kwa muda ambao haujulikani kulikuwa na Dimbwi la tope afu kwa pembeni kuna Bonde la maji ambalo wanyama wengi uja kunywa.
Kwayo naamini kuwa Wakati ule sikuwa na dhambi Mungu aliwafunga vinywa, Macho na hata pua wale wanyama wote msituni wasinifanye ubaya, Maana ingekuwa sasa labda hata mfupa wangu wale Maasai wasinge uona machoni pa dunia hii.
Naamini maneno ya Vitabu vitakatifu vya Mungu vilivyoandikwa sisi ni watawala wa Vyoote[emoji735]