Inamaanisha nini wananchi kumshangilia zaidi Mpina kuliko Rais Samia?

Inamaanisha nini wananchi kumshangilia zaidi Mpina kuliko Rais Samia?

Wananchi wa kisesa ni wajinga, wanashangilia changamoto lakini pia haohao hawajashangilia mafanikio yalipotajwa na Mpina.

Maana yake ni kwamba akili za watu wa jimbo la Mpina wanapenda kuona spana zikitembea badala ya chochote. ni ujinga tu.

Haya yote yanasababishwa na Mpina mwenyewe kashindwa kumjengea mazingira mazuri ya kisiasa mwenyekiti wake jimboni halafu anajidai kumnadi kwa ajili ya mwezi oktoba.

Ili chama kishinde uchaguzi bas kinahitaji cooordination na forged unit, Mpina hatambui hili badala yake anamuonea wivu Lissu anavyopashana na Mwenyekiti ama Raisi kimantiki majukwaani, so akiona changamoto kama za sukari basi anachangamkia fursa za kina lema na heche ili naye aonekane anaweza kuparurana.

anaingia kwenye mtego wa Chadema kuwataka wana CCM kukikosoa chama chao kichwakichwa ili kikose ushindi akidhani ataitwa shujaa kumbe anaua juhudi za chama.

Kama Mpina anatamani kuzungumza madhaifu ya chama chetu majukwaani basi, jukwaa stahiki halipo ndani ya CCM bali ni nje ya CCM, akiona vipi atimkie CHAUMMA.
 
Ukitoa kuchambana, mama ni mweupe hadi sio poa.
Sheikh watu wa Pwani wameshazoea taarabu na vichambo. Yaani ukimzingua tu, muda huo huo anaenda kuwasha redio na kukufungilia nyimbo za taarabu usikilize vichambo vyake.
 
Watanzania wameshaanza kuelewa yupi anasimamia upande wao na yupi mbabaishaji.Hawana haja ya 'mipasho' wala blabla
 
Mtasema yote ila huyo mama anamalizia kile kipengele cha katiba vizuri tu....ten years
 
Yaani nmeiona hiyo video, kusema kweli nimewaza saana kweli. Ukiachilia mbaali wananchi kukaa kimyaa wakata mh. Raisi akiongea, lakin namna alivyo muataki Luhaga unaona kabsaa picha kamili.
Wanawake wana tabia ya kujibu hoja kwa mihemuko na hisia.Fuatilia tu speech zake anapopelekewa hoja kinzani.Hawa watu hawana silika ya uongozi.
 
Habari wakuu,

Rais Samia anaendelea na ziara zake huko Kanda ya ziwa,leo kwenye moja ya mikutano yake huko ameraruana na Luhaga Mpina mbunge wa Kisesa.

Wakati Luhaga Mpina anazungumza wananchi walimshangilia sana kwa shangwe ila ilipofika wakati wa Rais Samia kuzungumza alimshambulia Luhaga Mpina akishirikiana na Waziri wake kilimo Hussein Bashe lakini wananchi walikaa kimya wakati wanampelekea mashambulizi Mpina.Je kitendo hiki walichofanya wananchi wanamaanisha nini?
They are fed up with her
 
Kosa ni kumdai miradi ya kimaendeleo kwa niaba ya Wananchi wake, alitakiwa amwage sifa ki-Lucas Mwashambwa na michozi ya furaha juu
Hahahah... Mkuu,... Kwa hiyo alikosea kudai maendeleo??.... Pale itilima naona penyewe mbunge kadai Barabara na akaahidiwa kupewa🤣🤣
 
Back
Top Bottom