Coolhigh
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 1,373
- 1,271
Kutua kawaida ni kwamba magurudumu yameshika ardhi kama inavyotakiwa. Kinachofanya ndege kupitiliza niHivi unajua kutua kawaida?kama imetua kawaida iweje itumbukie ziwani ??
1. Kutua nje ya eneo la kutulia. Mfano katikati ya uwanja kupelekea hatua zilizobakia ni chache kuweza kutosha kusimama.
2. Kutua kwenye uwanja ambapo upepo unaelekea upande ule ule ndege inapoelekea. Hivyo kusababisha ndege kwenda mbio zaidi ya inavytakiwa wakati ikitua.
2. Kutua wakati uwanja umeloa maji wakati kuna mvua au mara baada ya mvua kuisha. Hupelekea breki za magurudumu kutokuwa imara(kuteleza juu ya sakafu/lami)
4. Kuharibika kwa mfumo wa breki wakati wa kutua ( hydraulics ) na kusabahisha breki kutofanya kazi.