Tetesi: Inasemekana hii ndiyo sababu ya uhakika ya ajali ya ndege ya Precision Air

Tetesi: Inasemekana hii ndiyo sababu ya uhakika ya ajali ya ndege ya Precision Air

Japo ni tetesi lakini zina ulakini,kwani kulingana na abiria aliyekuwa ndani ya ndege,sio kweli kuwa ndege ilizunguka sana bukoba,ilijaribu kutua mala moja ikashindikana,akazunguka akaja kujaribu ,ndipo ikatumbukia ziwani.Hivyo mafuta yalikuwa bado yako mengi kwani alikuwa na mafuta ya kumfikisha mwanza.Kingine sio kweli kuwa hiyo ndege rubani ndio ameamua kuishusha ziwani,bali ndege ndio imedondoka,ghafla haya ni kulingana na maelezo ya rubani mstaafu,na ndio maana madhara yamekuwa makubwa kiasi hiki.Kwani kwa eneo alilokuwa amefika mita 100,kabla ya kukanyaga runway angeweza kuishusha majini pembezoni mwa ziwa hapo,na kusingekuwa na madhara kiasi hiki.Eti ipeleke ziwani tu watakuja kuwaokoa hahaaa!!ndege imekuwa lori la kulilaza kwenye mtaro,ili kupunguza madhara..
Sasa si bora hapo wamepatikana wengine wapo hai na maiti zimepatikana hyo ingetua nchi kavu asingetoka mtu pale.
 
Sasa si bora hapo wamepatikana wengine wapo hai na maiti zimepatikana hyo ingetua nchi kavu asingetoka mtu pale.
Ni kweli ila cha kumshukuru Mungu ni kuwa ndege imeanguka sehemu,nzuri,mfano kwa mbele kidogo kutoka pale ilipoangukia kuna kisiwa kinaitwa MUSILA,kama ingeenda kukigonga kile,sasa tungekuwa tunaongelea vifo vya mamia ya watu,kwani pale napo kuna watu wanaishi.
Ila kama ingekuwa ni utashi wa rubani kutua,kwa alipokuwa amefika,madhara yangekuww madogo sana.
 
Inchi ina mambo ya hovyo sn hii,,

Bila kuwajibishana ni kazi bure.
 
Hivi ndivyo jinsi ajali ya ndege ya Precion Air ilivyotokea:

"Ndege ilikua ikiongozwa na ruban mmoja hivi anaitwa Rubanga mwingne jina lake sijalifahamu vizuri. Tatizo ililopata mpaka ndege ikaanguka ni matairi ya ndege kugoma kutoka na unaambiwa senior captain alitoa taarifa Tower kuhusu hilo tatizo ila wakachelewa kujibu, ikabidi ndege izunguuke angani kabla ya kutua ili wapate uvumbuzi wa tatizo.

Baada ya kuona kimya rubani akapiga tena simu Tower na kuwaambia nipeni muongozo maana mafuta yataisha nimezunguuka sana, Tower wakamjibu ipeleke ziwani timu ya uokozi haitachelewa kuja kuwaokoa.

Sasa wakati wa kuipeleka ziwani rubani akaigonga kwenye mwamba na mpaka ndege inazama Tower taarifa walikuwa nayo, Cabin Crew wawili ilibidi waruke nje na ndio wakapata msaada kwa wavuvi na hata hao abiria 23 wa mwanzo waliokolewa na wavuvi na mitumbwi ila sio Tower wala Jeshi la uokozi, yaani wamewaambia waipeleke ndege ziwani watakuja kuwaokoa halafu hawakuja na baada ya polisi kuja wakawafukuza wavuvi waliokuwa wanawaokoa watu.

Ona jinsi polisi walivyo wazembe wamefukuza wavuvi waliokuwa wanaokoa halafu wao wakakaa pembeni eti wanalinda mali za raia.

Kusema kweli this accident hakuna mtu aliyetakiwa kufa kama uokozi ungefanyika mapema."

View attachment 2408808
View attachment 2408809
 
Back
Top Bottom