#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Kuongezeka kwa cases huko kunaweza kuhusishwa na janga la Uganda, ni kuzingatia tu njia za kujikinga zinazoshauriwa......mafua ya msimu hayajawahi kuleta crisis hadi ya kusababisha wagonjwa wengi wapate usaidizi wa kupumua kwa mashine ya oxygen.
Corona ipo toka mwaka jana na hatuchukui tahadhari hivyo ni akili ya kawaida tu kufikiri kuwa Tanzania kutakuwa na maambukizi kwa wingi na hivyo tungetegemea huo uhitaji wa mitungi ya oksijeni toka kitambo tu ila haikuwa hivyo hadi sasa ndio tunaambiwa kuwepo upungufu wa mitungi ya gesi na kuhusishwa na corona.

Hii imekaaje?
 
Ni vizuri kuwa realistic,sisi wote ni Watanzania tuwe na nia njema ikiongozwa na upendo kwa vizazi na nchi yetu.
Nilikuwa kwenye kongamano la dini la Wanaume (CMF) wa kanisa la TAG Jimbo la Mwanza kusini tar 2 na 3 Julai,wiki iliyopita.Tulikuwa watu wachache tu,tukapata taarifa mke wa aliyekuwa katibu wa Sehemu amelazwa Bugando ICU kwa changamoto za upumuaji,baadae akasimama Askofu wa Jimbo moja Singida akatuambia mume wa katibu wake wa kanisa amepelekwa Muhimbili yuko ICU kwa changamoto za upumuaji.
Kwanini natoa hizi facts?
1.Changamoto za upumuaji zipo.
2.Kwa kiwango gani?Ni Kama maleria?Hapana.
3.Twapaswa kuwa na hofu?Jibu ni hapana.
4.Mara zote kumekuwa na watu tunaoamini juu ya uweza uliojuu ya mwanadamu, ambaye ni Mwenyezi Mungu tumuombe aturehemu na kuiponya nchi yetu huku tukiwa na hekima pia ya kibinadamu.
 
Corona ipo toka mwaka jana na hatuchukui tahadhari hivyo ni akili ya kawaida tu kufikiri kuwa Tanzania kutakuwa na maambukizi kwa wingi na hivyo tungetegemea huo uhitaji wa mitungi ya oksijeni toka kitambo tu ila haikuwa hivyo hadi sasa ndio tunaambiwa kuwepo upungufu wa mitungi ya gesi na kuhusishwa na corona.

Hii imekaaje?
Mkuu mitungi ya oxygen mbona imeanza kuonekana kwenye mahospitali kitambo, kuna hospitali moja hapa Dar nilienda kutibiwa nimeshudia mitungi ya oxygen mingi tu inapitishwa pale reception, kwa hiyo unapoona mamitungi yamekuwa mengi sana, maana yake uhitaji wake nao umekuwa mkubwa. Ni nini sasa kilichopelekea huo uhitaji mkubwa, ndo hayo mafua ya msimu? au kuna cha zaidi....
 
Niko Mwanza na ninazunguka maeneo mengi kwa wiki, Shughuli zinaendelea kama kawaida.

Kwetu ni Igogo na nisehemu yenye population kubwa, sijasikia habari za watu kuugua korona.

Ninao marafiki kibao Kirumba, Malimbe, Igoma n.k, Na nisehemu zenye mikusanyiko mikubwa lakini hakuna habari ya korona huko pia.

Mahari napoishi pia sijasikia habari za ugonjwa wala vifo vilivyosababishwa na korona.

Pengine walipaswa watoe ufafanuzi vizuri kwa sababu si kwamba oxygen nikwajili ya wagonjwa wa korona pekeake.

Kwa uhaba huo wa oxygen na ugonjwa huu unavyoenea kwa kasi tayari majibu yangekuwa yameshaonekana mitaani (vifo kama ilivyo uko uganda)
Mmmh! Kumbe mpaka uone watu wakifa wengi? Alafu wakifa watarudi tena? Hilo sikubaliani na wewe, kinga ni Bora kuliko tiba na kifo maana uhai ni kitu muhimu sana.
 
Hata humu wamo wanaohamashisha huu uvumi. Gonjwa la kutengenezwa kuwaletea watu hofu.mbona mitaani hatuoni haya mambo?

Tetesi zinasema ni njia moja wapo ya kutimiza mashart, ukiona hivyo jua kuna kitu kinataka kukamilishwa kupitia mgongo wa covid
 
Mkuu mitungi ya oxygen mbona imeanza kuonekana kwenye mahospitali kitambo, kuna hospitali moja hapa Dar nilienda kutibiwa nimeshudia mitungi ya oxygen mingi tu inapitishwa pale reception, kwa hiyo unapoona mamitungi yamekuwa mengi sana, maana yake uhitaji wake nao umekuwa mkubwa. Ni nini sasa kilichopelekea huo uhitaji mkubwa, ndo hayo mafua ya msimu? au kuna cha zaidi....
Tatizo sio uwepo wa hiyo mitungi bali tunazungumzia huu upungufu kwa tafsiri ya kwamba uhitaji wa hiyo mitungi umeongezeka kuliko hali iliyo ya kawaida ndio kukatokea huo upungufu. Sasa kama ulikuwa unaiona hiyo mitungi toka mwaka jana pamoja na hii mikusanyiko ila hakukutokea upungufu wa mitungi,ndio nauliza kwanini sasa?
 
Inafurahisha sana kuona binadamu ambaye amezaliwa bila kuomba, amejikuta tu duniani anapambana kujaribu kukikwepa kifo.
 
Mnawatengenezea watu hofu,

Mtawapa pesa wakae ndani??

Au kwakua nyie mnampango wa kutumia Kodi zao Ili kununulia chanjo basi hamjali.
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
Nasema hivi tusitiane hofu, Mimi nipo Mwanza, na hayo unayozungumzia wengine ndio tunayasikia leo, hivi kweli ina maana hicho kirusi cha DELTA, ndio kwanza kimeingia TZ, kupitia MWZ?hiyo wave itapita tu kama yaliyopita mengine, cha muhimu ni kuchukua tahadhari zile za siki zote, hakuna haja ya kutishana!!kwani unaongea kama vile unashabikia kitu!!hao waganda/wakenya licha ya kuchukua hatua zote hizo nini kinaendelea?
 
Mnawatengenezea watu hofu,

Mtawapa pesa wakae ndani??

Au kwakua nyie mnampango wa kutumia Kodi zao Ili kununulia chanjo basi hamjali.
Nafikiri kinachosisitizwa ni tahadhari za kujikinga, ni sawasawa ukaambiwa chumba kimepuliziwa sumu wewe ukaamua tu kuingia ili ushuhudie kama kweli kuna sumu......je, endapo utaingia na madhara yakakupata kuna mtu utakayemlaumu, au utajilaumu mwenyewe. Kwa hiyo inapotolewa tahadhari fulani hakunaga muda wa mjadala, ni kufuata tu maelekezo ya hiyo tahadhari iliyotolewa kama amri ya jeshi. Kama ni uvumi itathibitishwa huko mbeleni kwamba ulikuwa ni uvumi.....
 
Eti " Hayawi hayawi sasa yamekuwa" bob nini cha kufurahia hapo kwa kauli yako hii?
Huyo jamaa inaonekana kama kuna ki mradi fulani anategemea kukifanya endapo masharti yakiongezwa labda watu kufungiwa ndani!!kwani sio kwa shangwe hilo
 
Malaika Mkuu John anailinda Tanzania huko aliko Behaviourist
Rafiki malaika mkuu John amekataliwa hadi huko mbinguni👇🤣
0000.jpg
 
Kwani nani alikuwa anatangaza hadi ujue kama kuna upungufu au hakuna
Ndio maana nikauliza hilo swali ili nijue kwamba huo upungufu ni sasa tu au toka zamani ila ilikuwa haitangazwi? maana humu mitandaoni tulikuwa tunaambiana kuwa hali ya corona ni mbaya na madaktari wanaujua ukweli ila hatukusikia kuhusu upungufu wa mitungi ya oksijeni kwa kipindi chote.
 
Ndio maana nikauliza hilo ili nijue kwamba huo upungufu ni sasa tu au toka zamani ili ilikuwa haitangazwi? maana humu mitandaoni tulikuwa tunaambiana kuwa hali ya corona ni mbaya na madaktari wanaujua ukweli ila hatukusikia kuhusu upungufu wa mitungi ya oksijeni kwa kipindi chote.
Toka kitambo maana ilikuwa marufuku kutoa taarifa na pia upuuziaji ulikuwa mkubwa kulingana na Serikali iliyokuwepo
 
Kipi ni ushahidi wa kwamba huo upungufu wa mitungi ulikuwepo toka zamani?
Unapenda ubishi? Kwani hujui kwamba serikali iliyopita haikujishughulisha na mambo ya Covid? Hata pesa walizopata walizipiga..Vifaa tiba alikuwa anakataa kwamba vinaleta barakoa.

Kama unataka ligi ya ubishi tafuta wengine.
 
Tuombe Mungu tu huku kwetu huu ugonjwa usije kwa nguvu,watu watapukutika kama kuku,hakuna anaejali kabisa huku mitaani,watu maisha yanasonga kama hakuna kinachoendela...
 
Back
Top Bottom