Inashangaza: Rais Samia mwezi Juni 2021 alisema akiba ya fedha za kigeni ni Dola bilioni 4,765

Tukiambiwa upinzani hatuna hoja tunakaidi. Sasa mpiga kura wa nakapanya huko mkienda kumwambia Rais alisema tuna akiba ya Dola Bilioni 4700 badala ya 4.7 atawaelewa kiasi awape kura kweli?

Hatuhitaji kura za wajinga, hizo tumewaachia nyie, sisi hizi hizi za waelewa zinatutosha na ndio hizi mnaua watu na kuwaacha na vilema vya maisha. Hatujawahi kujivunia wajinga hata siku moja maana tunachukia ujinga.
 
Siyo suala la propaganda wala nini. Ukweli mchungu ni kwamba serikali ya sasa haina umakini katika mambo mengi, tena muhimu. Tumepigwa kukubwa kwa kitu kizito chenye ncha kali!

#Mtanikumbuka!
 
Ya mara hii hakuwa amejiandaa kuongea na Taifa. Lissu alilazimisha wamuandalie hotuba.
 
Maana yangu ni kwamba kipindi hiki si wametoa taarifa kuwa wamekosea,mbona mwezi juni 2021 kama walikosea hawakutoa taarifa kuwa wamekosea?
Kwa sababu hakuna aliyegundua kuwa taarifa ilikosewa. Na wahusika nao, kwa bahati mbaya, hawakuona makosa hayo.
 
Ndio maana Magufuli mara nyingi alikuwa haandikiwi hotuba na alikuwa anakesha na mafaili mwenyewe
 
Mkuu raisi namba zinampiga sana chenga
 
Ok, hapa nimekupata; simply hizi taarifa zinatolewa kisiasa kuonesha hali yetu kiuchumi sio mbaya, kwasababu mwezi Juni watu hawakuhoji wakaona na mwezi Dec watudanganye tena ila ndio wakashtukiwa.
Binafsi naamini kosa hilo siyo makusudi, bali kosa la kitaaluma (gross professional mistake) kwa pande zote mbili--mwandishi na mwandikiwa. Simply, kuwa tatizo kubwa la elimu kwenye taasisi ya Urais, na uongozi kijumla.

Pili, kama ni makusudi, basi mwandishi wa hotuba atakuwa amefahamu fika engo ya udhaifu wa mwandikiwa, hivyo anamharibia makusudi. Maana yake ni kwamba mwandikiwa hatoshi kwenye nafasi yake, vinginevyo angeweza kupambanua makosa na kuyarekebisha mara moja.
 
Ikiwa mambo madogo Kama haya ya kusoma tu anakosea, vipi kuhusu mikataba?
 
Samia alirudisha mpaka mshauri wake binafsi wa uchumi lakini hajui ata inchi yake ina akiba kiasi gani uko chunguni japo anauwezo wakwenda ata kuangalia.
 
Point ipo
Raisi anashindwa vipi kutofautisha million na billion?
Achana hata na hilo. Anashindwa vipi kushtukia na kutambua nchi ina hazina kiasi gani, exactly? Maana sisi raia tumemwajiri Rais ili a-delive matokeo yenye viwango visivyoweza kutiliwa mashaka. Hivi angekuwa CEO au mkurugenzi mahali fulani, asingetumbuliwa jana yake, kabla hata hajafanya kosa?
 


Waandishi ndiyo wakulaumu hapa. Ni makoosa makubwa sana kuandika $4765 million badala ya kuandika $4.765 B au kwa ufupi $4.8B waandishi wa Tanzania wana complicates sana !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…