Dah umenikumbusha nakumbuka kwenye University niliyosoma kuna mtu nilimkuta na nilimuacha baada ya miaka kadhaa kupita nikasikia bado yupo chuo na issue ni kuwa amelogwa na watu wa kwao kuwa kamwe hatomaliza chuo kikuu apate degree yake so kila zikikaribia UE tu anaumwa kichaa yaani mpaka hospital ya chuo washamzoea. Nina ndugu yangu form 6 hakufanya vizuri so akaenda ualimu diploma, baada ya kumaliza ualimu akapata wafadhili fulani hivi wakimpromise kuwa watamsomesha degree ya 1 so akiwa anawasubiri akawa anafundisha, ka miaka miwili ikapita, akaona isiwe shida akaanzisha familia baada ya muda ndo akakumbuka kuwa bora aongeze elimu akasoma degree kumaliza akaaply hizo graduate trainee za bank fulani hivi akafanikiwa kupata kazi. So
Perry kwa kuwa umeenda straight kwenye kupata elimu na ukapata kazi faster usishangae mtu kuomba graduate trainee akiwa na 35 years! Kingine aisee kulogana kwenye baadhi ya familia za kitanzania kupo sana nafahamu watu wengi tu walikuwa na uwezo sana shuleni but mwishowe shule wakaacha maana ni full kuugua maradhi yasiyoeleweka full kupandisha mapepo sasa wapo kadhaa huwa wanasurvive tu kibishi bishi mwishowe ndo unamkuta mtu yupo 30s plus ndo anagraduate na then anaanza tafuta kazi. Aisee ikiwa kwenye ukoo wenu au familia/jamii yenu hamna issue za ulozi shukuru Mungu sana. Halafu
Perry mtu kuwa Meneja/Head of department aisee kuna vitu vingi hapo!! sio umri tu!! Ila hongera zako maana look like we mambo yako yanakuendea poa sana na soon utakuwa ni Meneja/Head of department mshukuru Mungu kwa hilo