Inasikitisha sana, kuna mtu ameomba kazi ya trainee akiwa na miaka 35

Inasikitisha sana, kuna mtu ameomba kazi ya trainee akiwa na miaka 35

Perry nakumbuka enzi zile ulivyojiunga na UDSM hatukulala humu.

Anyway, hongera kwa kupata ajira.
Hata mimi nakumbuka sana

Anaonekana ni jamaa ni majivuno na dharau

Yeye kufanikiwa kwa njia rahisi anahisi wengine ni vilaza (hatujui yeye kafanikiwi kivipi)

Aache kujifanya kama haijui Tz

Watu wana elimu safi tu still wan struggle hadi leo wapate ajira inayoeleweka yeye anashangaa kana kwamba kaja Tz jana.

Yeye kamshangaa jamaa wa miaka 35 ,mimi nimemshangaa yeye!!![emoji15]
 
Naona watu mmenielewa vibaya
Iko hivi,mimi sijadharau mtu,kilichonishangaza ni hii kuona mtu wa 35 years anaomba kazi ya Trainee,kwangu ni kitu kigeni kwa sababu nimezoea kuona watu wanaoomba hizi nafasi za kuwa Trainee ni vijana wadogo wa chini ya miaka 30.
Anyway jamaa kahudhuria usaili na tumeonana, I hope Mungu atamsaidia.
 
Bado unaendelea kuandika utumbo tu
 
Aisee!

Nakumbuka miaka hiyo ulipo kuwa pale jalalani (udsm) ukisoma electrial engineering wakala kichwa ukaja kuibukia kwenye economics!

Then ukasota sana kwenye ajira ..ukaenda TRA wakakula kichwa mwishoe ukaja ibukia kwenye ajira za serikali huko kigoma huko!

Leo umekuja unashangaa mtu kuomba ajira akiwa na miaka 35! Kweli dunia inakimbia kwa kasi!
Hahahahaha jamaa anadhani tumemsahau na tambo zake za udsm
 
Inasikitisha kwasababu wewe una kazi tayari....ila kiuhalisia ni suala la kawaida hapa nchini
Huo si ukawaida. Stop normalizing matatizo yaonekane ni normal. That not normal

Thats is state ya ajira nchini ilivyo enda chini.
 
Naona wana wamekushambulia sana kwa hii post yako mkuu. Sasa ili kuwaonyesha kuwa we unaelewa situation ya mwana basi msaidie huyo mwana apate internship na ikiwezekana mpambanie apate ajira kabisa.
Hilo ndio la msingi sio kushangaa
 
Watanzania tuna matatizo sana.kwa hiyo kitu kama ni kigeni kwangu siruhusiwi kushangaa,kisa nitaonekana nadharau watu?
Bado unaendelea kuandika utumbo bora unyamaze tu, kwahiyo ukija huku uswahilin kwetu ukaona watu wanakula ugali kwa dagaa kila siku wiki nzima utakuja hapa kuanzisha uzi kisa kwenu mlo mmoja tu una mboga saba?
 
Ndio maana ukienda ulaya nao wanashangaa inawezekana vipi sisi waafrika tunanaishi under 1 dollar kwa siku.
Kwa hiyo tusifundishane maisha,kitu kilicho strange kwangu kinaweza kikawa ni cha kawaida kwa mtu mwingine and vice versa.
Hakuna mahali nimeonyesha kumdharau mtu hapa kwenye huu uzi kama mnavyojaribu kuonyesha.
 
Boss wangu alikua kanipa kazi niwapigie watu waje kwenye interview ya kazi ya Trainee iliyotangazwa hapa ofisini kwetu miezi kadhaa iliyopita.

Surprisingly katika kupitia cv zao, nimeona kuna mtu ana miaka 35 nae kaitwa. Nimejiuliza huyu mtu wenzake wa umri huo sasa hivi huenda wamefikia levels za umeneja au head of departments. Sasa huyu ndio kwanza anaomba Trainee.

Nimesikitishwa sana.
Mungu kamuandikia kila mtu njia yake

Usisikitike

Mnaweza wote mkatangulia kaburini na mkamuacha anaendelea na maisha yake
 
Back
Top Bottom