Inawezekana kipindi cha Mkapa ndio ujambazi mkubwa ulitamalaki

Inawezekana kipindi cha Mkapa ndio ujambazi mkubwa ulitamalaki

Zamani kuipata pesa ya serikali ilikuwa ni ngumu sana ndo maana kukawa na magenge kutoka kwa viongozi sasa hivi watu pesa wanachota tu unakuta kijana mdogo ni tajiri mkubwa na ni mtoto wa kiongozi hizo pesa katoa wapi
sasa hivi watu pesa wanachota tu unakuta kijana mdogo ni tajiri mkubwa na ni mtoto wa kiongozi hizo pesa katoa wapi😭
 
Na alitangaza hadharani, majambazi wanyang'anywe silaha harakaharaka. Alitoa ile kauli kimzahamzaha ila kumbe alimaanisha.

Baada ya hapo stori zikawa ni mwndo wa majambazi yauawa wakati yakijaribu kupambana na polisi. Yani kama wewe ni jambazi unawekwa kwenye rada, unakamatwa unapelekwa milimani/maporini unapigwa shaba kisha asubuhi na mapema unakuwa kwa niuuuuz
Kipindi hicho ilikuwa mtuhumiwa wa ujambazi akidakwa na polisi analazimishwa aende porini akaonyeshe wenzake walipojificha halafu wakifika porini mtuhumiwa alikuwa anajaribu "kutoroka" na kupigwa risasi "miguuni" zinazompelekea kupoteza maisha
 
nasikia watuhumiwa wengi walikua wanatoka mara serikali ikatumia njia ya kuwapa kipaumbele jeshini na upolisi sasa ivi hali ikawa shwari.

ukichunguza ni kama kweli 70% ya polisi na wanajeshi ni watu wenye vina saba vya mkoa wa mara
Hapa umechanganya kabisa Mura matukio kama hayo yanahusishwa na WACHAGA .
Wakuria wa zamani ukiwawekea Begi la pesa na ng'ombe kwamba achague cha kuiba,atachagua ng'ombe!
Wakuria tupeni habari za cattle rasling na sio money heist
 
Na alitangaza hadharani, majambazi wanyang'anywe silaha harakaharaka. Alitoa ile kauli kimzahamzaha ila kumbe alimaanisha.

Baada ya hapo stori zikawa ni mwndo wa majambazi yauawa wakati yakijaribu kupambana na polisi. Yani kama wewe ni jambazi unawekwa kwenye rada, unakamatwa unapelekwa milimani/maporini unapigwa shaba kisha asubuhi na mapema unakuwa kwa niuuuuz
Hii ilikuwa idea nzr saana
 
Magufuri ndo alikuja kufuta ujambazi

Nakumbuka sana ilikuwa ikifika saa kumi na mbili jion kutoka busisi ferry kwenda sengerema kabla hujafika nyampande kutekwa ilikuwa lazima wala siyo ombi
Kilichokuja kufuta Ujambazi ni Technologia..

Mambo mengi ya Ajabu yameondolewa na Technologia kwa asilimia kubwa.
Zamani watu wanaiba sana Kwasababu kwanza mambo yalikuwa gizani(hakuna umeme wa kutosha taa zinawaka mwanga mdogo) bado hakuna camera, bado hakuna data za kuweza kufatilia fedha mtakazoiba.
Zamani watu wanaiba simu mambo yanakuwa freshi tuu. Sa hivi hata kuiokota simu ni kama umeokota matatizo.

Ila leo ukiiba tatizo linakuja utadakwa tuu mfumo ukiamua kukutafuta. Njia za kujua upatikanaji wa wahusika zimekuwa rahisi

Sa hivi ujambazo umehamia kwenye kitu kinaitwa Utapeli na watu wasiojulikana. Na ni kwa vile hatujafikia hatua nzuri za technologia yakuondoa hayo. Mfano kuwe na Camera kila kona ya mji haya mambo ya wasiojulikana huwezi yasikia

Pia
Watu wamekuwa wakitapeliwa sana japo ni kwa vile hatujapata watu(police) walioko makini kwenye kuwatafuta hao matapeli
 
Uvamizi vituo vya polisi na tukio moja kujaribu kumnyang'anya askari wa kike wa JW akiwa lindoni ilikuwa wakati wa JK na mwanzoni mwa kipindi cha JPM.
Ujambazi wa kuvamiwa magari na kuwekeana magogo road, migodini ni kipindi cha Mkapa,.
Ujambazi kwenye bank, magari ya fedha, bureau de change, na mitaani wakati wa Mkapa na JK.
Wakati wa JK mitaani kwenye viduka, majumbani tulivamiwa sana hadi mchana kweupe. Wakati huu peak ya matukio ilikuwa juu hata kesi ya akina Zombe kilitokea siku moja na ujambazi wa kiwanda cha BIDCO ndipo wale wauza madini wakasingiziwa majambazi wa hilo tukio.
JPM alikuja kumaliza matukio yote haya. Watu walishuhudia mchana kweupe Jambazi anawawaiwa na kukamatwa na askari pale Ubungo Kibo(Rombo) alikuwa ndani ya gari ndogo limeegeshwa. Akawekewa mashine begani, wazee wakammiminia njugu begani. Wakamkagua akakutwa na bastola mbili kiunoni.
Hiyo ilikuwa mubashara jua linawaka raia wanaona. JPM na Sirro combo hatari sana, kiboko ya wahalifu(majambazi).
 
Kipindi cha Samia walianza Tena watu wakapaza sauti. Ndipo wazee waka copy kazi ya Sirro na JPM mambo yakapungua.
Kama kawaida zikaanza kelele, wazee wakapunguza kasi kuwapora silaha wahalifu na kuwapitia majumbani mwao hadi usiku.
Eti unafuatwa kisha kesho linafika tangazo ulijaribu kupambana na wazee wakakuzidi nguvu wakakupeleka kwa muumba haraka. Hii inaitwa Sirro & JPM style ya kuwanyang'anya silaha majambazi.
 
Njia ya kwenda chunya makongorosi ilikuwa haipitiki usiku mchana mkipita salama kushukuru tulikuwa hatuendi home kabisa
 
Hakika magu aliwamaliza thugs.kuna jamaa yangu nae alikua yupo yupo tu home na wife yake lakini alikua anaishi vizuri mno kumkuta mguuni katupia buti la laki na ushee kawaida tu.kumbeeeee alikua jambawazi nlikuja jua siku walipouwawa majambawazi kama watano hivi nae akiwemo.aiseee haya maisha yana siri nyingi sana bro mshana
 
Siku hizi si salama kuvamia na kukimbia na gari au pikipiki , zamani maboda boda kulikuwa hakuna sasa hivi ukiiba watakimbiza na pikipiki hadi wanakukamata. Mazingira yamebadilika.
Kuna boda inaweza kufukuza defender, discover, Vogue au land cruiser yoyote, sema advantage yao miaka hiyo magari hayakuwa mengi hivyo jam ingekua sio kikwazo kwao tofauti na miaka hii foleni kuanzia asubuhi hadi jioni
 
Kilichokuja kufuta Ujambazi ni Technologia..

Mambo mengi ya Ajabu yameondolewa na Technologia kwa asilimia kubwa.
Zamani watu wanaiba sana Kwasababu kwanza mambo yalikuwa gizani(hakuna umeme wa kutosha taa zinawaka mwanga mdogo) bado hakuna camera, bado hakuna data za kuweza kufatilia fedha mtakazoiba.
Zamani watu wanaiba simu mambo yanakuwa freshi tuu. Sa hivi hata kuiokota simu ni kama umeokota matatizo.

Ila leo ukiiba tatizo linakuja utadakwa tuu mfumo ukiamua kukutafuta. Njia za kujua upatikanaji wa wahusika zimekuwa rahisi

Sa hivi ujambazo umehamia kwenye kitu kinaitwa Utapeli na watu wasiojulikana. Na ni kwa vile hatujafikia hatua nzuri za technologia yakuondoa hayo. Mfano kuwe na Camera kila kona ya mji haya mambo ya wasiojulikana huwezi yasikia

Pia
Watu wamekuwa wakitapeliwa sana japo ni kwa vile hatujapata watu(police) walioko makini kwenye kuwatafuta hao matapeli
Tek sio tatizo.marekani wana tek ya hali ya juu lakn ujambazi na mauaji vinafanyika tu
 
Back
Top Bottom