Uvamizi vituo vya polisi na tukio moja kujaribu kumnyang'anya askari wa kike wa JW akiwa lindoni ilikuwa wakati wa JK na mwanzoni mwa kipindi cha JPM.
Ujambazi wa kuvamiwa magari na kuwekeana magogo road, migodini ni kipindi cha Mkapa,.
Ujambazi kwenye bank, magari ya fedha, bureau de change, na mitaani wakati wa Mkapa na JK.
Wakati wa JK mitaani kwenye viduka, majumbani tulivamiwa sana hadi mchana kweupe. Wakati huu peak ya matukio ilikuwa juu hata kesi ya akina Zombe kilitokea siku moja na ujambazi wa kiwanda cha BIDCO ndipo wale wauza madini wakasingiziwa majambazi wa hilo tukio.
JPM alikuja kumaliza matukio yote haya. Watu walishuhudia mchana kweupe Jambazi anawawaiwa na kukamatwa na askari pale Ubungo Kibo(Rombo) alikuwa ndani ya gari ndogo limeegeshwa. Akawekewa mashine begani, wazee wakammiminia njugu begani. Wakamkagua akakutwa na bastola mbili kiunoni.
Hiyo ilikuwa mubashara jua linawaka raia wanaona. JPM na Sirro combo hatari sana, kiboko ya wahalifu(majambazi).