Mpuuzi sana huyo, kumbe ndiye chanzo kikubwa cha kuhujumu mradi huu mkubwa ambao ungeleta fahida kubwa kwa Taifa letu si kwa ujenzi wa Bandari tu bali na ujenzi wa viwanda vikubwa na vyenye maana kwa ustawi wa Taifa letu.
Nimemsikiliza kwa umakini alicho kuwa anaeleza - tangu mwanzo alionekana yuko overly biased against Chinese kwa kuwasimanga mambo chungu mzima eti hawa ni mabepari,wajanja,wanakuja Kaliakoo kuuza pety products,mara wachina wa sasa tofauti na walio jenga reli ya TAZARA,eti kafanya upelelezi wa miradi iliyo tekelezwa na wachina nchi za nje akagunduwa ni balaa tupu as if huu ndio ungekuwa mradi wa kwanza wa wachina kuwekeza kwenye ujenzi na uendeshaji wa Bandari kwenye mataifa mengine,anarudia propaganda zile zile za mataifa ya magharibi za kujaribu kuwa demonise wachina, si ajabu alikuwa greased kuhakikisha mradi huu will never see light of the day.
Kakoko asitake kubabaisha watu, wachina na waarabu wa Oman walitaka kuja Tanzania kuwekeza katika mradi wa kujenga na kuendesha masuala ya Bandari na viwanda vitakavyo zunguka Bandari, hakuna popote wachina walisema wanataka kuingia ubia na Serikali yetu kujenga na kuendesha Bandari - Serikali haitachangia hata senti tano kwenye mradi huo, sasa kwa nini watu kama Kakoko atake kushauri Serikali kujiingiza kwenye uendeshaji wa Bandari ambayo hawakuijenga au kuwekeza zaidi ya kuwapatia aridhi ya kujenga.
Wachina wa uwekezaji katika Bandari wangekuja kama Wachina wenzeo waliowekeza kwenye viwanda huko Mkulanga, sijawahi kusikia Serikali ikiwaiingilia kwenye uendeshaji wa viwanda vyao,sana sana Serikali inacho pashwa kuhakikisha ni ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wawekezaji - sasa kwa nini uwekezaji kwenye Bandari uwe tofauti na uwekezaji kwenye viwanda - au Kakoko alikuwa na wasi wasi kwamba ujenzi wa Badari kubwa ya Bagamoyo kutampuguzia wadhifa na influence yake kwenye masuala Bandari nchini ndio maana kashirikilia hoja ya ukodeshaji wa aridhi kama ndio hoja kubwa ya kuhujumu ujenzi wa Bandari ya B'moyo kwa kuwasingizia Wachina eti wanataka kupora aridhi kwa muda mrefu na kuiingizia hasara Taifa letu - Kakoko hasemi chochote kuhusu modalities zinazo tumiwa na Serikali kuwapatia aridhi wawekezaji wa kwenye viwanda, je, wanalipa pango la aridhi na kwa muda gani.