Inawezekana kujenga nyumba hii kwa millioni 14

Aisee!
 
Fundi wangu kani ambia vyumba viwili na sebule kama hii million 14 inatosha na mimi naogopa hela ikatike njisni nibaki pagale ushauri wenu wadau.

View attachment 1965447
Weka mlango wa mbele na malizia choo cha ndani na piga rafu nyumba yote. Usisahau kuchimba shimo la majitaka moja kwanza. Baada ya hapo vingine utamalizia ukiwa ndani
 
Umetisha engineer...u apatikana wapi nikupe m25 unijengee
 
Weka mlango wa mbele na malizia choo cha ndani na piga rafu nyumba yote. Usisahau kuchimba shimo la majitaka moja kwanza. Baada ya hapo vingine utamalizia ukiwa ndani
Ndivyo nataka
 
Umetisha engineer...u apatikana wapi nikupe m25 unijengee
Ahahah sisi kazi zetu za kuhama hama! Ww anza tu mkuu mwenywe tutapeana ushauri humu humu! Ujenzi ni gharama ila sio kama watu wanavyotishana also watu wengi wanaingia gharama unnecessary kwa kutoshauriwa vizuri especially kwenye ramani.
 
Nafikiri kingine ambacho watu hua hawashauriwi vizuri ni kuhusu bati, sasa hivi umeingia mtindo wa hizo bati almaarufu kama msauzi, hizo bati bila kujali gauge yake watu wanaweka tu kwasababu ya fashion but unaweza kuweka bati zile za kawaida/za kizamani zenye gauge 28 na nyumba/paa likaa muda hata wa 30 years but again bei yake hizo bati sio mbaya kiviile kama hizo za Msauzi ambazo zinauzwa kwa piece while hizo za kawaida inauzwa kwa bando; hili jambo mhandisi mwenzangu, hebu tuwaambie watu waelewe hasa hao wanao anza kujenga sasa hivi, i mean hawa ambao ndio wanaanza maisha.
Kuna rafiki yangu tulikua tunajenga nae nyumba, spead yetu ya ujenzi ilikua sawa, mwenzangu alikua nje ya nchi anamtumia mkewe pesa za ujenzi, mimi nipo hapa hapa Bongo halafu show nasimamia mwenyewe, wakati wa kupaua yeye akabandika hayo ya msauzi na mimi nikanunua bati la Alaf la kawaida but gauge 28, nyumba yake kabla ya miaka 2 kupita tayari zile bati zimepauka sana but kwangu kawaida tu, linazidi kung'aa. Labda kama utakuja ichukulia mkopo bank hiyo nyumba then hilo la MSAUZI litaongeza thamani ya nyumba (valuators wengi wanaangaliaga vitu hivyo) ili uchukue mpunga wa maana, hivo tu.
 
Acha uongo, hizo bati migongo mipana haifiki 50000.
Hata alaf wenyewe wanauza 37,000
Mkuu, umesoma maelezo vizuri? Inategemea na mahali, muulizaji haja specify sehemu alipo, wewe umefanya hitimisho kwamba yupo Dar right? Rudia tena nilicho andika then kosoa kistaarabu. Halafu kingine ni hiki, migongo mipana gauge ngapi???? Ubora wa bati sio aina ya mgongo, sio mwanamke huyo kwamba utaangalia kama ana tackle au laa, ubora wa bati ni gauge!
 
nakushauri anza hela nyingine utaipata bila kutarajia ya kumalizia hiyo nyumba. alichokwambia lakini kina ukweli pia we nanza tu
 
hahaaa haiwezekani kamwe nondo zenmyewe sasahivi 25000 badala ya 22000 au 23000 huyo jamaa anataka kukuua na presha tu hapo ilipofika kama haina blandering wala gypsum inaonekana si chini ya 25 amini maneno yangu
 
Poa
 
Mlipe mtaalam laki tatu akutengenezee BOQ, utakuja kunishukuru.

Zingine zote ni porojo tupu.
Hata wao bado miyeyusho nilimpata mmoja Kala laki bado haja Sema ni bei halisi ni ngapi
 
Hata wao bado miyeyusho nilimpata mmoja Kala laki bado haja Sema ni bei halisi ni ngapi
Acha masihara bana, BOQ hawasemi bali unaletewa in writing.

Hiyo laki moja mlipeana tu pesa ya bia, hata hiyo laki tatu nimekwambia ni ya kishkaji.

Ni bora ikugharimu pesa kidogo kwenye BOQ ukawa na uhakika na unachokifanya au ukajipa muda zaidi wa kujipanga.

Hawa local fundi wetu kwenye estimation usiwaamini, asipokununulisha material nyingi zaidi basi utanunuwa pungufu na bado material zaidi zitahijika.

Last month nimefanya ukarabati mdogo tu home fundi wa tiles kaninunulisha tiles zimebaki box saba karibu laki mbili nzima hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…