Inawezekana kujenga nyumba hii kwa millioni 14

Inawezekana kujenga nyumba hii kwa millioni 14

Mimi ni fundi, baadhi ya mafundi wasio na weledi huwa wanamtajia Boss gharama za chini ili aingie kichwa kichwa apate kazi,akishaanza kuchimba msingi na kuleta cement na tofali hapo ndio fundi ataanza nunua hiki mara nunua hiki ambavyo ndivyo vinakuja kukutoa nje ya reli na kulala na viatu huku pagale hata kuezeka bado achilia mbali grill/plasta.
Umemjibu vizuri mkuu
 
Eneo lenyewe la kuhamisha udongo . Njiro
 
14m unaweza kuhamia kabisa lakini sikuhakikishii kama itakuwa imefikia hatua hiyo ya lipu kwa gharama za vifaa vya ujenzi kwa sasa
 
Na jaribu December wakati wa vacation
Hapo tofali nunua kabisa
Tofali 3500 mpaka za choo
Cement 35. Mpaka choo unatumia
Nondo 34 unafunga mkanda wa chini na lenta na choo cha upana wa futi 6 mzunguuko
Kokoto chukua mende hiyo itamaliza mpaka kufunika shimo la
Mbao za kufungia mkanda juu na chini lazima ukodi weka 150k kukodi na sahani utaongezea
Mchanga mende nne zinamaliza mpaka plasta
Madirisha mpe fundi kwa jumla na mlango kwa hii ya chuma dirisha moja moja utapigwa na kitu kizito mbao nyumba km hiyo 2by2 55 na 4by2 70 hizo usinunue zenye dawa kabisa utakuja kufa huku uamini kama umepigwa chukua oil chafu kwenye gereji halafu mpe mtu au paka mwenyewe zikiwa chini na siku fundi akianza kuweka kenchi panda juu na upake oil kila anapokata, misumali nk nunua au piga hesabu kwa meters za nyumba yako
Fundi wapo wazuri kwa bei nzuri tu na usimpe fundi kwa rejareja mpe full kuchimba mpaka tofali tatu za juu shimo unauza lote kuchimba mpaka kufunika
MAFANIKIO MEMA
 
Huyo fundi atakuua! In fact hiyo gharama ni kubwa sana, kwani kiujenzi, matofali mia nne (400) unapata chumba kimoja cha vipimo standard! Kwa vyumba viwili ni matofali mia nane (800) na sebule labda kwa vile ni kubwa basi kisia matofali mia nane (800) kwa hiyo ni matofali 1600 au shilingi 1,600, 000/=. Haya wengine dadavueni hiyo gharama kutoka kwenye taarifa yangu hii. Asanteni.
Msingi tu wa hiyo nyumba unaweza kuwa tofali 800-1000
 
Hapo tofali nunua kabisa
Tofali 3500 mpaka za choo
Cement 35. Mpaka choo unatumia
Nondo 34 unafunga mkanda wa chini na lenta na choo cha upana wa futi 6 mzunguuko
Kokoto chukua mende hiyo itamaliza mpaka kufunika shimo la
Mbao za kufungia mkanda juu na chini lazima ukodi weka 150k kukodi na sahani utaongezea
Mchanga mende nne zinamaliza mpaka plasta
Madirisha mpe fundi kwa jumla na mlango kwa hii ya chuma dirisha moja moja utapigwa na kitu kizito mbao nyumba km hiyo 2by2 55 na 4by2 70 hizo usinunue zenye dawa kabisa utakuja kufa huku uamini kama umepigwa chukua oil chafu kwenye gereji halafu mpe mtu au paka mwenyewe zikiwa chini na siku fundi akianza kuweka kenchi panda juu na upake oil kila anapokata, misumali nk nunua au piga hesabu kwa meters za nyumba yako
Fundi wapo wazuri kwa bei nzuri tu na usimpe fundi kwa rejareja mpe full kuchimba mpaka tofali tatu za juu shimo unauza lote kuchimba mpaka kufunika
MAFANIKIO MEMA
Mkuu naomba maneno yako yatafsiri katika namba basi ili tuone, usisahahu kutueleza ni bei za Mbagala, Wazo au Kigamboni.
 
Mwamba unaweza weka ramani ya nyumba yote na view yake kwa pande zote
 
Fundi wangu kani ambia vyumba viwili na sebule kama hii million 14 inatosha na mimi naogopa hela ikatike njisni nibaki pagale ushauri wenu wadau.

View attachment 1965447
Inategemea na maeneo uliopo lakini kwa gharama hyo hatakama upo maeneo gani ya nchii hyo pesa haitoshi...,,, watachakachua hyo nyumba ndani ya miaka 10 itaonekana kama jumba la miaka 50 kwa uchakavu, ushauri wangu tenga walau m 30 ndio utaweza kuimaliza hyo nyumba hadi finishing uweze kuamia
 
Haya ukiongeza na hizo za msingi ni kama 2.6mi/=.
Sasa kama tofali tu ni 2.6m, ukiweka saruji, nondo, kokoto,mbao,bati,mchanga,labor,gharama za fundi,umeme,maji, plumbing,gharama za kukodi vifaa, kuchimba shimo la choo, fundi wa kupaua bado tu hyo m 14 ipo?
 
Back
Top Bottom