Inawezekana kupika rosti/mchuzi mzito bila nyanya.

Inawezekana kupika rosti/mchuzi mzito bila nyanya.

Nipo kwenye group ambalo ukitoa nyanya, kitunguu, karoti na hoho jikoni sijui kitu 😁
Ila naamini Wakali wa michemsho, karanga na viungo vingine wanaweza. Haya JF sweethearts ambao huwa mnasema jikoni mpo vizuri. Challenge hii kwenu sasa 🔥🔥
Usiwaze sana mkuu, ukiongezea nazi hilo ndilo group kubwa zaidi la wapishi bongo.
 
Wapika rosti ya kiswahili, mchuzi au makange wamekariri sana kuweka nyanya nyingi ili kuifanya rosti au mchuzi kuwa mzito na wenye ladha nzuri. Kwa wajuzi wa mapishi wanaweza kupika mchuzi mzito kabisa bila nyanya hata moja.

Inawezekana...

Tumia ama tui zito la nazi au tui la karanga kutegemea na aina ya mboga au unga wa starch au viazi ulaya vilivyopondwa au viungo mboga vilivyosagwa na kuwa rojo kama hoho nyekundu, pia waweza weka binzari kwa ajili rangi na seasoning (spices) nyingine kwa ajili ya ladha kwa kadiri ya ladha uipendayo...
 
Attachments

  • IMG-20241230-WA0001.jpg
    IMG-20241230-WA0001.jpg
    85.3 KB · Views: 5
Yeah inakuwa tu vizuri, Nilijaribu xmass makange ya samaki sikuweka nyanya na ikatoka tu poa

Makange ya namna hiyo huitwa "changamoto", sijui waswahili hutoa wapi majina ya vyakula 😆

Uko vizuri Lee isipokuwa chips umewahi kuziopoa, bado zina mafuta pia ungeweza kuzifanyia unyade zaidi kwa kuziwekea unga wa paprika kupata karangi

Screenshot_20241230_115533_Chrome.jpg
 
Wapika rosti ya kiswahili, mchuzi au makange wamekariri sana kuweka nyanya nyingi ili kuifanya rosti au mchuzi kuwa mzito na wenye ladha nzuri. Kwa wajuzi wa mapishi wanaweza kupika mchuzi mzito kabisa bila nyanya hata moja.
Kuna michuzi ya kihindi/Kipersia mingi mno ambayo haitumii nyanya.

images (68).jpeg

Chicken korma,

Hata ukitoa wahindi sisi watu wa Pwani tunatumia sana Nazi badala ya Nyanya, kuna michuzi ya Nazi mizito unatumia tu Nazi za packet bila maji, na boneless chicken ama fish.
 
Kuna michuzi ya kihindi/Kipersia mingi mno ambayo haitumii nyanya.

View attachment 3188481
Chicken korma,

Hata ukitoa wahindi sisi watu wa Pwani tunatumia sana Nazi badala ya Nyanya, kuna michuzi ya Nazi mizito unatumia tu Nazi za packet bila maji, na boneless chicken ama fish.

Huu mchuzi umewekwa coconut milk na butter cream (hii ni nzito)...
 
Makange ya namna hiyo huitwa "changamoto", sijui waswahili hutoa wapi majina ya vyakula 😆

Uko vizuri Lee isipokuwa chips umewahi kuziopoa, bado zina mafuta pia ungeweza kuzifanyia unyade zaidi kwa kuziwekea unga wa paprika kupata karangi

View attachment 3188484
Ahhh changamoto wanaweka pilipili nyingi na vitunguu vingi sana. Vitu ambavyo sivipendi

Ila mkuu umejulia wapi kupika maana Mimi nikiona mwanaume anajua kutumia binzari, sijui ajina moto, huwa namuweka directly katokea pwani

Au kuna njia zingine maana kuna time naona bora nichemshe nyama ina tangawizi na ndimu, ugali unaenda maana sina alternatives za kuepuka mikaango😁
 
Back
Top Bottom