The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Possibly, unaandika out of ignorance wa kutoisoma na kuielewa Katiba y JMT Ibara ya 37 (3).CDF amesema wazi kabisa hata walipo muamuru waziri mkuu aje hawa ku-disclose information.
Kitu cha msingi cha kujiuliza ni kwanini magufuli alihisi yuko comfortable kuwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi kuliko wanasiasa wenzake!?
CDF anasema walimhamishia mzena kupunguza watu walio kuwa wanamuona.
Hebu isome hapa 👇👇 halafu uniambie wewe unaelewa nini hapo.
37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.
(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na
masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha
Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na
shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa
kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama naye hayupo au ni mgonjwa,basi; (c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
Hebu nipe maoni yako katika haya mawili;
1. Wewe unaelewa nini katiba inaposema "endapo kiti cha Rais kiwazi tokana na sababu nyingine yeyote?" Hiyo sababu nyingine yoyote unadhani ni ipi? Je, Rais kuugua au kuumwa kiasi cha huyo Rais kushindwa kutekeleza majukumu yake haiwezi kuwa sababu ya hawa waliotajawa katika Ibara ndogo 3 (a), (b) na (c) kuchukua majukumu ya Rais kwa maoni yako?
2. Na Je, wewe unaelewa nini katiba inaposema "......shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao...?". Kwani wewe hizo shughuli za Rais ni zipi kama sio hizo zilizotajwa na katiba Ibara ya;
"..... 33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu...?"
Ndugu Duc in altum, ni wazi kuwa hujui usemalo.(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b) Mwisho makamu wa raisi ni mshika mikasi tu kikatiba mpaka anapo apishwa kuwa raisi.
Jeshi hali mtambui makamu wa raisi kwenye chain of command CFF alisema raisi inabidi aapishwe kwa gwaridwe vinginevyo jeshi halita mtambua.
Kwanini Pm na General secretary ataarifiwe hao ni watendaji na ndio wanao husiko ku-organise hayo mambo mengine ya taratibu zinazo takiwa.
Do you have any supporting evidence ya Ibara yoyote toka kwenye katiba ya JMT ya mwaka 1977 ku - justify hiki ulichokiandika hapa?
Why don't I say that, you are writing out of your own ignorance?
Soma tena na tena Ibara ya 37 yote ya Katiba ya JMT ujipe ufahamu...