Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Possibly, unaandika out of ignorance wa kutoisoma na kuielewa Katiba y JMT Ibara ya 37 (3).

Hebu isome hapa πŸ‘‡πŸ‘‡ halafu uniambie wewe unaelewa nini hapo.

37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.
(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na
masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha
Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na
shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa
kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama naye hayupo au ni mgonjwa,basi; (c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano
.

Hebu nipe maoni yako katika haya mawili;

1. Wewe unaelewa nini katiba inaposema "endapo kiti cha Rais kiwazi tokana na sababu nyingine yeyote?" Hiyo sababu nyingine yoyote unadhani ni ipi? Je, Rais kuugua au kuumwa kiasi cha huyo Rais kushindwa kutekeleza majukumu yake haiwezi kuwa sababu ya hawa waliotajawa katika Ibara ndogo 3 (a), (b) na (c) kuchukua majukumu ya Rais kwa maoni yako?

2. Na Je, wewe unaelewa nini katiba inaposema "......shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao...?". Kwani wewe hizo shughuli za Rais ni zipi kama sio hizo zilizotajwa na katiba Ibara ya;
"..... 33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu...?"
Ndugu Duc in altum, ni wazi kuwa hujui usemalo.

Do you have any supporting evidence ya Ibara yoyote toka kwenye katiba ya JMT ya mwaka 1977 ku - justify hiki ulichokiandika hapa?

Why don't I say that, you are writing out of your own ignorance?

Soma tena na tena Ibara ya 37 yote ya Katiba ya JMT ujipe ufahamu...
 
Mkuu tuseme wewe ndio unajua katiba
Mtu anayepaswa kulitaarifu baraza la mawaziri kuhusu afya ya raisi ni nani!?
Je ni CDF!?
Ni katibu mkuu kiongozi!?
Waziri mkuu!?
Au makamu wa raisi!?
CDF alitakiwa ampe nani taarifa ili alitaarifu baraza la mawaziri!?
 
Mkuu tuseme wewe ndio unajua katiba.
Hata wewe ukitaka kuijua katiba, unaweza kuijua. Tatizo lako ni kuwa hutaki kutaka kujua.

Hata tu kusoma na kuelewa Ibara ya 37 niliyokutupia uisome umeshindwa kufanya hivyo. Ungeusoma na kuielewa utaona majibu ya maswali yako yote haya uliyouliza..
Mtu anayepaswa kulitaarifu baraza la mawaziri kuhusu afya ya raisi ni nani!?
Je ni CDF!?
Ni katibu mkuu kiongozi!?
Waziri mkuu!?
Au makamu wa raisi!?
Katika mfumo wa utawala wa nchi yetu, ni wazi kuwa ingalau unaelewa Rais ndiye mkuu wa nchi na serikali, au siyo?

Baada ya Rais, who is the second from the top miongoni wa hawa watatu uliowataja? Ukijibu vyema swali hili, utakuwa umejijibu na swali lako uliloniuliza..!
CDF alitakiwa ampe nani taarifa ili alitaarifu baraza la mawaziri!?
Who is CDF katika mfumo wa utawala wa nchi yetu? Huyu ni ofisi nyingine independent inayojitegemea huko. Anapaswa kusubiri maelekezo tu toka kwa Mkuu wa nchi, serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hawa CDF, IGP na DGIS walichokifanya kuanzia ugonjwa hadi kufa kwa Rais Magufuli ilikuwa ni kinyume cha utaratibu wa katiba. Kwa lugha rahisi ni kuwa, walivunja katiba.!

By the way, katika ofisi ya Rais, yupo katibu binafsi wa Rais na yupo Katibu kiongozi na Katibu wa Baraza la mawaziri. Kwa yahusuyo afya ya Rais, yupo Mganga mkuu wa serikali na yupo daktari/jopo na madaktari binafsi wa Rais..

Hawa ndio wanaoweza ku - chain taarifa zozote zinazomhusu Rais za kiafya na general capability yake ya kutenda majukumu ya ki - Rais kwa Vice President (a second official person in command ktk mfumo wa utawala wa nchi/serikali yetu).

Naye atafuata procedures kama katiba inavyoelekeza katika Ibara ya 37(2)

Na upande mmoja ipo familia ya Rais. Hujiulizi ni kwanini familia ya Rais Magufuli ilitengwa na hawa watu kuanzia kuugua hadi kufa kwake na badala wakashirikishwa kwenye mazishi tu?

Soma katiba uelewe kuwa katika wote wanaotajwa kuwa wanaweza kuchukua nafasi ya Rais endapo Rais hayupo nchini, au mgonjwa au kiti chake kipo wazi kwa sababu yoyote ile iwe ni ugonjwa au kifo, CDF hayupo katika orodha hiyo..!

Ni vyema ukaitafuta katiba, kisha soma sura au sehemu ya pili yote ya Katiba ya JMT inayofafanua kwa undani "MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO
WA SHUGHULI ZA SERIKALI".
Kila swali lako lina majibu ya kina hapo..
 
Mkuu mbona unajibu kihuni
Flow ya taarifa kuwa raisi hajiwezi kupelekwa kwa baraza la mawaziri inafanywa na nani!?
Kwanini hutaki kukubali kuwa katiba imeacha gap haisemi chochote!
Anayepaswa kumpa taarifa makamu wa raisi ni nani!?
Usiniambie nisome katiba nijibu hauoaswali wewe mjuvi
 
Kama ni makamu anapewa taarifa kwanza kabla ya baraza yeye anapewa na nani!?
Kwa hiyo katiba yako na ulete na vifungu ku-justify hilo kama ulivyo fanya awali.
 
Suala la Samia kutokuwa na taarifa au kutaarifiwa juu ya afya ya Rais Magufuli ni uwongo!!
alikuwa anajua kila kitu,wanatuzuga tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…