Habari wakuu
Hapa nilikuwa naweka ligi ya mabishano, hivi inawezekana kweli watu walioingia mjini hapa 1992 mpaka leo 2021 Hana hata kiwanja cha kuzugia kweli, enzi hizo maeneo ya Tegeta, Goba, Kawe, Bunju ilikuwa mapori matupu unafika unafyeka nyasi na kujipa eneo mwenyewe.
Mbaya zaidi ulikuwa ukitaka hata kiwanja cha jero pale Ubungo unapata, Sasa mtu ananiambia kaja DSM 1992 lakini tunaganga njaa hapa, imenibidi nitafakari kidogo.
Nimesikitika sanaa.
Uzi tayari ...!
Maisha ni chaguo lako.
Mimi nina babu yangu ( late ) alikuwa Askari Magereza Ukonga, alinunua eneo kubwa tu kama nusu eka Mombasa Ukonga na ndio amejenga hapo.
Ila nina Anko zangu kama wawili.
Hawa MaAnko zangu, Babu wa Magereza ndio aliwasaidia kupata kazi huko huko Magereza.
Wa kwanza yeye alinunua kiwanja Ukonga huko Moshi Bar kitambo sana, wakati bado yuko Magereza akawa akipewa wafungwa wakafanye kazi za jela, anawafanyisha fasta, halafu anawapeleka kwenye kiwanja chake wanajenga.
Siku moja moja kama kawaida, amewapeleka wameloweka zege na kama kaqa, zege halilali. Mpaka usiku hajarudisha wafungwa kambini. Alivyogundulika alifukuzwa kazi ila ana sehemu ya kuishi.
Mwingine yeye kazi huwa anasema aliacha mwenyewe. Tangu miaka ya 90 yuko Dar amepanga tu, dereva daladala lakini hana hata gari la kazi la maana. Anadandia tu.
Hivi karibuni ndio mwanaye mmoja wa kike alipelekwa huko Oman kufanya kazi za ndani, akawa amenunua kiwanja Chanika na kujenga nyumba.
Basi Anko huyo ndio anakaa huko, ukimkuta kijiweni anawatambia madereva wenzio kwamba ,wajiongeze siyo kukomaa tu kwenye magari kizembe, yeye amejengaπ€£π€£
Hayo ndio maisha ya waswahili.