Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Roho wanawekaje kwenye miti? Hapo ndo nachanganyikiwa kabisa!
Haya ni mazindiko ya kiafrika, roho haikai kwenye mti ila anafanya zindiko anaungana na ule mti ukitaka kumuua ni mpaka ule mti ufe kwanza. Hizi zilitumika kama kinga enzi zile watu wanatekwa maporini safari za miguu hamna magari. Zipo nyingi ambazo nimewahi kuziona in action ni kama;
1. Dawa ya mbio- hii kulikuwa na jambazi sugu wanamtafuta kila wakija akitoka mbio hata mbwa hawafati hiyo speed ya jamaa.

2. Kukosekana kwenye hatari- hii mtu akija akudhuru anakuwa hakuoni, walihangaika na huyo mtu mpaka wakaamua kuua mwanae kwa hasira baada ya kumkosa muhusika kila wakati.

3. Dawa ya kurusha ngumi- hii ukimpiga mtu ngumi anazikwa, inafanya kazi pale tu unapokuwa unaonewa lakini ukianzisha ukorofi utapigwa kama ngoma.

4. Dawa ya kurusha jiwe au fimbo - hii kama mtu kakukimbia na huwezi mpata basi ukichukua kitu chochote ukarushia uelekeo wake humkosi, hata awe mbali wa viwanja 3 vya mpira.

Na zingine kibao kwa nyie watoto wa miaka ya 90 na 2000 hamuwezi elewa.
 
Sahihi
 
Nendeni, hao waliowapigia simu wanajua, sasa wanawaonea huruma ndio maana wanawaambia muende msije mkafilisika na bado mgonjwa asipone!
 
Kuna mwamba kpnd nipo mdogo alikua mwizi, na alikua akikamatwa akipigwa hafi, watu wanakata panga inaonekana kaumia ila kumbe wanakata gogo! Wanamwacha hapo kama kazirai hivi kesho yake mwamba anadunda.
 
Hizi mambo kweli zipo sema, ndo ivo siku hizi kama vile haziamniki, mm sijawahi shuhudia na kuona zinafanyikaje ila kipnd nipo mdogo ilikua sio jambo la ajabu kuskia...
 
Hii nilishuhudia pia jamaa mwizi Kaishapigwa zaidi ya mara 8 minadani na hafi akiumizwa analazwa hospital tu anatoroka anarudi zake kujiuguzia ghetto siku kadhaa anarudi jobπŸ˜€πŸ˜€
Kuna mwamba kpnd nipo mdogo alikua mwizi, na alikua akikamatwa akipigwa hafi, watu wanakata panga inaonekana kaumia ila kumbe wanakata gogo! Wanamwacha hapo kama kazirai hivi kesho yake mwamba anadunda.
 
Nishawahi kusikia hii, kuna wengine ni mpka uwaanike juani ndo wakate moto
 
Hii nilishuhudia pia jamaa mwizi Kaishapigwa zaidi ya mara 8 minadani na hafi akiumizwa analazwa hospital tu anatoroka anarudi zake kujiuguzia ghetto siku kadhaa anarudi jobπŸ˜€πŸ˜€
Mm mwenyewe nashangaa mbona hawapo sku hizi? Ujue hiyo ni fursa kabisa? Au ilikua ni nguvu za mwili na matambiko?
 
Teknolojia zetu waafrika zimekaa kiajabu ajabu hata kujifunza mtu unajikuta unaogopa,hiyo noma roho ipo kwenye mti dah...
Hakuna ajabu yoyote ila ni elimu, hio haina tofauti na uhai uliofichwa kwenye sindano na vidonge kwani usipochomwa au kumeza unakufa na ukitumia unapona.
Hivyo kuna tofauti gani na aliyelinda uhai wake kutumia mti?

Nikupe mfano mwingine,
Huyo mzee hata ingetokea ajali asingekufa kirahisi, Je ipi teknolojia bora kati ya hiyo ya kujikikinga na miti au vitu na teknolojia ya Airbag ambayo inapunguza risk wakati wa ajali?
 
Mimi naamini kwa 100%
Kwetu Mpimbwe huko Katavi wilaya ya Tanganyika mila hii ipo.
Sio mti tu, kuna maji, mnyama, mmea, shallow graves n.k.
So sishangai huyo ndugu yako kusema hayo.
Mie mwenyewe siku nikiamua kuzindika mwili wangu, naenda tu home kwa bibi, mambo yanakuwa safi.
Sema masharti yake ndio yananishinda
 
Zama hizi si wazee tu au wenye umri mkubwa.
Hata rika la balekhe wanafanyiwa.
 
Yesu....πŸ™†β€β™‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…