Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Tunajenga kwa pesa zetu za ndani kumbe alikuwa anatupiga na kukopa kimya kimya
 
Daah.... Sasa km anakuwa bado anaongea si unamuacha akae milele?
Waafrika tutapata lini akili ya kuthamini vyetu?
Huko Asia kuna baadhi ya makabila wanatunza maiti za wapendwa wao na huwa wanafanya sherehe kuzitoa ndani na kuzipamba.
Sisi tunashindwa kutunza mtu anaeongea,?
Eti kisa anaoza, acha aoze tuone mwisho wake!
 
Nilishashuhudia huu utopolo. Mtu katafunwa na kansa ya jicho, jicho lote limeng'oka limebaki shimo tu ukiangalia hata ubongo unaweza kuuona halafu shimo liko infected limeoza lakini jamaa hafi. Mpaka madaktari wanashangaa kwa sababu hali aliyokuwa nayo ni ile wanaita medical impossibility!

Mpaka akaja mdogo wake akawatonya kuwa watoboe paa hapo alipolala ili apigwe na mwanga wa jua hasa jua la saa 6 mchana. Kweli wakafanya hivyo na japo alikuwa kwenye coma jamaa alijitikisa; na hata siku moja hakumaliza akafariki. Bila kufanya hivyo sijui ingekuwaje.

Mwafrika bado ana hizi hekaheka. Imagine mtu unajifanyia madawa ili usife hata uugue vipi. Na Mungu naye kwa vile si Athumani ndiyo unatandikwa na kansa. Unaishia kujitesa si wewe tu bali na wapendwa wako. Mambo mengine hayafai!🚮
 
Duh kazi kwelikweli,nahisi huyo mzee atakuwa msukuma maana ndo mambo yao hayo atawasumbua sana nyie nendeni tu ili lisije kujirudia kwa mmoja wenu..
SUKUMA GANG mnisamehe mweeh 🤣
Kama ni usukumani sishangai kule Kuna mambo aisee ukiyasikia na kuyaona unabaki kinywa wazi
Wasukuma jamani tunaingiaje hapa tena? Jiiizozi! 😁😁😁🖐
 
Kwanini hamkupeleka wataalam wajifunze kinachoendelea? Mwili umeoza, hauwezi sapoti uhai ila mhusika yupo hai, badala ya kuita dunia uchunguzi ufanyike ni kwanini mnatoboa paa afe. Hamkuona umuhimu wa sayansi kwenye jambo kama hili?
 
Sasa unataka ushauri wa Nini na wakati umeshaambiwa muende Kijijini mkakate huo mti?humu hakuna atayekushauri la maana
 
Ukitaka kusoma kuhusu dawa unasoma unajua parasetam sijui ampicplini, hiyo ya miti kwanini inapatikana kwenye hadithi tu?
 
Bora kuficha roho kwenye mti...
 
Hii tafsiri inaishia anga la Afrika tu si ndio?

Maana kule kwa wenzetu Mila zao zinaitwa Dini, marehemu wao (mizimu kwetu) wanaitwa watakatifu.

Na huu ujuzi wa kwamba mila na tamaduni hizi ni kuingia mikataba na shetani umeupatia wapi?
Wenzenu wanaziandika kwenye kitabu kila mtu ajisomee. Za kwenu zipo kwenye hekaya.
 
Haya matukio yangekuwa yanatokea kweli yangekuwa yameshavuta wawekezaji. Hii dunia matajiri, viongozi, watu wenye nguvu adui yao ni kifo. Wangeungana wajue ni nini hicho.
 
Wajinga wajanja?hiyo hata mzungu haijui hiyo dadek
Ujanja uko wapi? Wewe unajua namna ya kucheza na mauti ila nchi na jamii yako watu wanakufa mahospitalini, vichanga vinakufa huku wewe unaificha hiyo elimu halafu uwe mjanja? Mzungu akijua namna ya kutibu analeta kwa jamii yake mpaka huku inafika, anaandika na kitabu.
 
Watu wenyewe si ndio nyie wabishi na wajuaji,mmekumbatia vya mzungu na kuviona Bora na kuvidharau vyenu, endeleeni kunywa mseto,waacheni wanaoupenda Uafrica wafiche roho zao kwenye miti
 
Kwani unataka tuanze kukuelezea namna wazungu walivyoua mila desturi na tamaduni zetu, na kisha kuweka mifumo ambayo itatulemaza milele?!
 
Watu wenyewe si ndio nyie wabishi na wajuaji,mmekumbatia vya mzungu na kuviona Bora na kuvidharau vyenu, endeleeni kunywa mseto,waacheni wanaoupenda Uafrica wafiche roho zao kwenye miti
Ujinga tu. Binadamu mwenye akili akiwa na elimu yenye manufaa anaiweka hadharani, kwenye vitabu, mashuleni. Sasa wewe una jambo lako unalifichaaaa unakufa nalo halafu uonekane mjanja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…