Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao?

Akili ya mtu inapimwa kwa kipimo gani?

Ujinga wa mtu waupima kwa kipimo gani?
 
Kwa katiba hii CCM itatawala milele,ila mambo yatabadilika, mbaya ya CCM ni shule za kata! Vijana wamesoma na wanajielewa,ikikaa vibaya watalia bila kupenda na watakimbiana .
 
Kaka paschal naona umeanza kufilisika MTU HACHAGULIWI KWA SABABU YA JINSIA YAKE ANACHAGULIWA KWA KUJENGA HOJA /UWEZO WAKE WA KIUTENDAJI.

wajinga pekee ndio hupiga kura za kumchagua eti kwa sababu ya uanamke wa madame Samia.

Akishinda Samia iwe SABABU YA UWEZO KIUTENDAJI na sio uanamke wake.

Wasalaam

Kwa Sasa kijijini MPUMBWI.
 
Hapo sijajua kama umetumia elimu Yako,au uchawa.
Ifikie hatua ukue mkuu.

Tunakuheshimu sana,great thinker.
Ila kwa Sasa karibu kufatilia jamaa flani anaitwa sijui Mwafambwa sijui Mwashamba.
Ambapo mnaweza mkawa mnafanana kwa Kila kitu.
Mda mwingine msipelekeshwe na unazi,bali uhalisia wa mambo.

Hao unaowaita wajinga,ndo kioo chenu ulimwengu.
 
Tuendelee kukataa wanawake sababu wanaume wametupa maendeleo makubwa sasa TZ ni kama mbinguni 😂
 
Unasema umepigwa na bumbuwazi, basi jiandae kupigwa na pumbuwazi, yahani unatushauri tuchague ujinga kisa mwanamke, si ndio hawa bwana Balthazar Engong Engonga kawapelekea Moto, ndio unatushauri tuwapeleke ikulu

Mwambieni bibi yenu bahati haiji mara mbili hiyo nafasi ilikua tu ni zari sasa akajiandae kurea wajukuu
 
Mkuu great thinker iweje unaanza kampeni za mapema, ni kwa faida ya nani labda?

Je wasio na imani na tawala za kike hawaruhusiwi kutofautiana na wewe?

Wamarekani siyo wajinga, ni watu walioadvance sana kielimu.

Utendaji mbovu na udhaifu wa kiuongozi wa wanawake around the world umemnyima ulaji Kamala.

Raia wa Usa washaona na kujifunza madhaifu ya tawala za kike na kuona kwamba hazifai, ref to Bangladesh, Tz nk nk kote wanakotawala wanawake.

Imani za wananchi kuhusu uongozi wa kinamama imeshuka sana kwa kutumia 'shamba darasa' la kuwatazama wale waliojaliwa kuongoza namna wanavyoboronga wawapo madarakani
.
Labda kuna afueni kidogo kwa nchi zenye strong constitution, kuwabana wafuate sera za nchi na si vinginevyo.
 
Sarcasm
 
Wamarekani wengi wàna akili sana, watanzania wengi ni wajinga sana. Ndio tofauti kubwa
 
Vituko vyako unavyo hadi uzeeni?Vimebadilika na kuwa vibweka.
 
Mkuu P nafikiri wenzetu walishatoka kwenye kura za huruma. Wanachagua mwenye mikakati wanayoitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…