Infosys IPS (T) LTD wakanusha kuhusika na LUGUMI katika kashfa ya ubadhirifu

Ndio awa tunasema wanacheza muziki wasoujua ilimradi mmeambiwa mcheze basi mnacheza tu. Kampuni imefanya kazi hii miaka minne nyuma sasa hapo Kitwanga alikuwaje Waziri!
 
Usamehewe
 
Haya sasa ukweli umewekwa wazi kumbe ni juhudi za kumpiga vita Waziri Kitwanga na kutaka kuichafua serikali ya Magufuli.

Wapiga dili tafuteni kiki nyingine ukweli ndio huu.
Jamani, hata kabla mafaili hayapitiwa tayari jitihada za kumsafisha zinazizima! Mmmh
 
Hayo maelezo hayajamchafua wala kumsafisha Kitwanga, yameonesha kuwa anaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja na kashfa hiyo. Uchunguzi zaidi unahitajika.
Hata hivyo, integemea anayehoji ana lengo gani, kuweka mambo ya msingi wazi au kuyaficha ili kujenga picha tofauti.
Anayehoji anatakiwa asiwe na upande bali awe anatetea maslahi ya uma.
 
Za Kuambiwa changanya na zako
 
Haya sasa ukweli umewekwa wazi kumbe ni juhudi za kumpiga vita Waziri Kitwanga na kutaka kuichafua serikali ya Magufuli.

Wapiga dili tafuteni kiki nyingine ukweli ndio huu.
Umekuwa mwepesi kweli kutetea. Acha facts plus evidence vifanye kazi zake.
 
Hivi hii bado ni trailer au movie tayari imeshaanza...
 

Hakuna cha vijana kutumika ktk siasa wala nini!

Kama hawa watu mnaojaribu kuwatetea leo hawana uhusika wowote, hizi sarakasi zote za nini eti!!??

Kwa nini watu wanapojaribu kuhoji jambo hili ambalo lina kila dalili ya ufisadi wa kutisha pengine kuliko hata wa Bandari mnawasema "vijana acheni kutumika kisiasa??"

Tunachotaka watu ni kuona haya mapambano ya ufisadi kupitia kauli mbiu na vibwagizo vya "HAPA KAZI TU" na "UTUMBUAJI MAJIPU" yanafanyika kwa uwazi na kwa kila mtu bila kujali ni nani!!

Halafu unajaribu kututoa kwenye hoja ya msingi kwa kumwingiza Lowassa na CHADEMA yake kwenye ishu ya mkataba wenye kila dalili ya ufisadi wa Lugumi Enterprises vs Polisi vs huyu Kitwanga. Unadhani kuwa sisi ni wajinga sana wa kiwango chako siyo??

Well, hata kama Lowassa na CHADEMA wanahusika kwa namna moja au nyingine na kampuni hii, tunataka hatua zichukuliwe mara moja kama inavyofanyika ktk matukio mengine!!
 
Acha upotoshaji na mihemko kuna mafisadi zaidi ya CCM? Hizo 37 billion shs waliolipwa bila kumaliza kazi wahusika hawana connection na uongozi wa CCM? Katika wanafiki na wapiga debe umeshika bendera, anzia EPA, ESCROW, rada, meremeta, IPTL, UDA, nk, hebu niambie wahusika ni wanachama wa chama gani? Ni nani waliokuwa kwenye dhamana ya hazina yetu? Haya au na wewe ni buku 7? Unatumia nguvu nyingi kutaka kusafisha tuhuma kama kawaida yenu.

CAG, na sasa kamati za bunge zinashughulikia wewe unaleta upambe fisadi mkubwa na mafisadi wenzako wa Lumumba
 
Jambo lilikuwa rahisi km lisingekuwa na ufisadi, ilikuwa ni kubeba mkataba na kuupeleka kwenye kamati muda ule ule. Leo ndo mnaanza kukanusha, halafu mnawaambia watu wanachuki mnawafanya hamnazo nyinyi ndo wajanja. Kuna watu wenu deal mliwakwepa issue yote wanaijua hata mfanyeje wanatatoa info kidogokidogo, sana sana mnampa kazi mkuu wa kaya.
 
Hao ni vibaka kama vibaka wengine ukishaona wameibuka leo wadhajianda au wamesafisha ushahidi kitambo, ila subiri tuone.
Uko sahii. Hiyo ni Fraud kwenye level ya juu sana. Kama huna muono mzuri huwezi kuuona. Ila kuna tatizo somewhere.

Uhusiano wenyewe uko hivi>>>>>>>>>>>>

KITWANGA(Wazirir wa Mambo ya ndani)=INFOSY=AFIS(BIOMETRIC-Wizara ya Mambo ya Ndani)=LUGUMI=UFISADI wa 34bil

Kutokana na uhusiano huo, na ili uchunguzi uweze kuwa wazi na huru, ni bora Waziri(Kama Mstaarabu) ajiuzuru.
Kimaadili KUNA TATIZO HAPO la Conflict of Interest
 

Uko sahii. Hiyo ni Fraud kwenye level ya juu sana. Kama huna muono mzuri huwezi kuuona. Ila kuna tatizo somewhere.

Uhusiano wenyewe uko hivi>>>>>>>>>>>>

KITWANGA(Wazirir wa Mambo ya ndani)=INFOSY=AFIS(BIOMETRIC-Wizara ya Mambo ya Ndani)=LUGUMI=UFISADI wa 34bil.

Kutokana na uhusiano huo, na ili uchunguzi uweze kuwa wazi na huru, ni bora Waziri(Kama Mstaarabu) ajiuzuru.
Kimaadili KUNA TATIZO HAPO la Conflict of Interest
 
Hawataki kutuambia Lugumi kwa nini amelipwa hela kabla hajamaliza kazi? Kwa nini nguvu kubwa inatumika kumtoa mwenye hisa mwanasiasa Kitwanga na ufisadi uliofanywa na kampuni yake? Kitwanga kama Waziri mwenye dhamana alichukua hatua gani kuzuia, kushughulikia, kuhakikisha na kuwakamata wahusika kama yeye hahusiki?

Wanalazimisha watu wote wawe wanasifia tu kama majuha, leo wameuchukua mkataba toka kwenye kamati ya PAC na kuuhamishia kamati ya Adadi, mara wanasema hakuna ufisadi wowote katika mkataba kati ya LUGUMI na jeshi la Polisi, jitihada kubwa kuficha ukweli za nini?
 

kiukweli hakuna mtu anaweza kukimbia hapa Tanzania...na wala kujificha....ila inawezekana ikafanywa hivo kwa uangalizi "maalum" na maelekezo "maalum"

Unakumbuka kashfa ya Meremeta Ilifichwa vipi?
 
Ndio awa tunasema wanacheza muziki wasoujua ilimradi mmeambiwa mcheze basi mnacheza tu. Kampuni imefanya kazi hii miaka minne nyuma sasa hapo Kitwanga alikuwaje Waziri!
Nyerere alisema''....tuliwatimua kazi pale tu tulisikia uwepo wa tuhuma fulani dhidi ya viongozi wetu.....''
 
Kesi ya Ngedele unampa Nyani, unategemea nini?
 

hivi unaujua uhusiano wa kindugu uliopo kati ya adaddi na Mwemah?

Ndugu yangu ......sasa ndio tunapata picha halisi ya maigizo ya serikali ya CCM
 
Tupo pamoja mkuu, sijui hujanielewa wapi. Issue ya Lugumi, Lugumi ndio direct client kwa Polisi, Lugumi kapelekea tenda ya supply and install kwa waamerika (Biometrica), Biometrica kusupply vifaa na kumpa kazi ya kuinstall Infosys ambayo kati ya wamiliki wake, Kitwanga yupo. Kwa trend hii, Infosys inakili kupokea $74,000.00 kutoka Biometrica kwa kazi aliyoifanya.

Issue yangu kubwa hapa ni vijana kujaribu kututoa kwenye reli, kujaribu kuiondoa Lugumi na kumtwisha mzigo Kitwanga.
 
Mbona hii imekuja baada ya kuhakikisha mkataba hautoki bali unapelekwa kwa kamati ya ulinzi na usalama? Ambayo mkuu wake alikuwa polisi? Kwa nini haikutoka mapema... na je wabunge wa kamati ya ulinzi wanakula kiapo tofauti na wabunge wa PAC kwamba wao wanaaminiwa zaidi? ONLY IN TZ....
 
Jamaa kajichanganya mara hawana uhusiano na Lugumi, mara tulipofanya utafiti tukagundua lugumi aliwapa kazi biometrica...

BTW, huyo anayemhoji meneja anaongea kama Mzee Mwanakijiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…