sijui umekula maharage ya wapi wewe?
ila nahisi ni Yai la kuchemsha kisha umeshushia mtindi.
kwanza kabisa nikujulishe tu, Dinho Magic alibeba tuzo ya Mwanasoka bora wa Dunia pindi ambapo Dunia ina wachezaji kwelikweli. timu zilikuwa nondo na wachezaji walikuwa nondo haswa. makipa walikuwepo, mabeki walikuwapo, viungo ndio balaa, washambuliaji ndio usiseme...
Totti, Del Piero, Raul, Figo, Eto'o, Rivaldo, De Lima, Beckham, Owen, Mendieta, Valeron, Riquelme, Efenberg, Gerald na wengine wengi aliwabwaga. Saint Gaucho aliweza kupiga chenga za maudhi na kuwadhalilisha mabeki visiki waliokuwa kwenye soka miaka hio, na sio hawa mabeki wenu wa siku hizi kila wakiruka kichwa wakitua chini basi kitu cha kwanza ni kujitoa doksi.
Dinho Magic amesambaratisha viungo imara vya timu tofauti hapa ulimwenguni. Dinho ameshatoa assist za ajabu na hazijatokea mpaka leo. Mfano ni ile pasi aliomtengenezea Nesi na kisha Nesi kukiri kuwa hata angefumba macho basi mpira ule aliopewa na mjanja wake basi ilikuwa afunge tu na kuweka kumbukumbu yake ya goli la kwanza kuifungia Barca alipewa pasi na Mtume na Nabii wa Mwisho wa Soka.
na unapojishushia heshima ni pale unaposema eti Mtakatifu Gaucho angekuwepo kwenye kipindi hiki cha Ronaldo na NESI basi asingefanya lolote...
nikukumbushe tu matukio muhimu. Dinho Magic aliwahi kuja Sansiro na kuikuta Milan dume dume kweli, lakini alichotufanya ilibidi Berlusconi amtume Uncle Fester aangalie uwezekano wa Nabii huyo kuja kuvaa uzi wa Rosoneri.
Nesi wako unaemsifia wewe hajawahi kufunga goli la move Nesta akiwa anamkaba. Nesi mara zote alizokabwa na Nesta amefunga magoli ya penati tu.
huyo Ronaldo alishakuja Sansiro enzi za mbavu Cafu mbavu Maldini na alijambajamba matokeo yake mwishoni akataka eti kumpiga Cafu...
siku nyingine alikuja Sansiro kisha akakutana na Brigadia jenerali mstahafu Ivan Rhino Genaro Gatuso na cha moto alikiona.
so usijidhalilishe kwa kulinganisha kipindi cha Gaucho na kipindi hiki cha kwako wewe na wanyoa viduku wenzio.
jifunze kupitia kwa sisi tuliokuzidi kijana.
unapobishana na Belo na Balantanda ukae ukijuwa utalemaa hapohapo na hutokuja kujuwa.