Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Sasa itakubali vipi bila ya kuwasha data [emoji856][emoji856][emoji856][emoji856]data ni tofauti na bando ...washa data bila ya bando kisha washa vpn ..ngoma inakonecti
Umeelewa nilipoquote lkn au umekuja tu kujibu yangu?
 
Mkuu, jaribu kuwauliza google kuwa infinix hot 10i zina uwezo upi kwenye battery, ukikuta ni 6000 mAh rudi hapa uweke like, kisha upita kimyakimya wanaozijua simu wasije kukucheka!
We ni mgonjwa kumbe sasa infinix ni simu? Brand zote kali nazijua ndo mana nikamalizia mwishoni kwa kuandika bila shaka ni wanzuu nikimaanisha tecno, itel, infinix..ndo watumiaji wake wanapenda mserereko sababu sio rahisi ukute mtu ana macho matatu anahangaika na Free internet
 
Kuna mtu anatumia vpn na inaspidi maana naona ni Kama mwendo wa kobe
 
Nimetumia hizo wire turn, thor etc lakini nilikuja kuona naichosha tu simu yangu maana zina run background, network bandwidth ndogo, slow internet connection mwishowe simu ina struggle sana ku access internet inaishia kupata moto kuliko kawaida yake. Kwanini maisha ya betri yasipungue!
Ni usumbufu sana, vyabure vinagarama zake
 
Hello wanajamii forums,

Ni wiki kama mbili sasa tokea kutumia zile apps za wire tun, Thor VPN na HA Tunnel zinazotoa huduma ya free internet kutoka servers za mbali kama vile UK, US, German e.t.c

Simu yangu iliyotoka kiwandani ikiwa na 6000 mAh, ambayo ilimaliza siku 3 pasipo kuchajiwa kwa matumizi ya kawaida pasi na kuwasha data, au masaa 40 kama nitaacha data on! Sasa imegeuka nahisi si zaidi ya 1400 mAh. Mwanzoni wakati naanza kutumia hizo huduma, simu ilichemka kuliko kawaida, kuna wakati niliiweka kwenye friji ili ipunguze joto, maake nilihisi ingelilipuka. Nimetumia kwa muda sasa kiasi kwamba simu ilichukua masaa sita tu kuwa na chaji. Ndipo nilipoamua kufuta app hizo! Mbali na kuchukua hatua hiyo, simu yangu inatunza chaji kwa muda wa masaa nane tu, niwashe data, nisiwashe data, niitumie, iwe screen off, niizime, nisiizime! Haya yote yamekuwa bure! Masaa nane tu ndio yaliyobaki kuniweka hewani! Vya bure vimeniponza!No free lunch in America
 
Back
Top Bottom