Mkuu mimi si mtoto mdogo, i need reasons nishaona propaganda nyingi za kusifia Apple ila unaongea na mtu ambaye ameanza kumiliki simu kabla ya iphone kutoka,
Nimekuuliza maswali hujajibu hata moja. Nafafanua zaidi.
1. Ni kweli sio quantity bali price pia, kampuni ambayo ilikuwa inasifika kuuza simu za bei rahisi za 30,000 ghafla wateja wake wamechukuliwa na kampuni inayouza simu mamilioni ya Hela ina make sense kwako? Hebu tumia hata 1% ya brain,
unachoongea hapa ni kama unasema soko la machinga limeuliwa na super market za masaki na Obey ghafla watanzania hawavai mitumba na nguo za kichina bali wanavaa jeans na tshirt branded.
2. Highend za Nokia zilitumia Open source kuanzia 2004 Maemo mpaka 2011 Meego, Simu kama N9, N900, N800, N810 etc zilitumika na Mahackers mbali mbali, Watu wanaorun distro mbalimbali za Linux, watu wanaocode na mambo mengi ya super users, so unataka kuniambia hawa watu ghafla wakaacha kuwa super user na wakaenda jela ya Ios?
3. Symbian pia ilikuwa ni maarufu kwa watu wanaopenda kutumia simu kwa matumizi makubwa, kudownload movies, miziki, magame mbalimbali, emulators, kucustomize simu, themes etc mambo haya hayakuwepo iphone na huwezi ukatoka kwenye hivi vitu ukaingia jela na kuwa sawa.
Hakuna hata mmoja anaeweza kuprove iphone imeiua Nokia ni Blah blah na Propaganda za kimarekani tu.
Lete reason hapa.