Serikali inaweza kuchukua hatua na inaona kinachoendelea lakini kwa namna fulani serikali inanufaika na ilo suala kwaiyo inafumbia macho na kufanya tu danganya toto za hapa na pale ionekane inafuatilia. Nchini mwetu tatizo la umasikini na ukosefu wa ajira ni kubwa sana kama serikali ikitokomeza hao makahaba je itaweza kuwatoa kwenye lindi la umasikini? itaweza kuwapa ajira mbadala?. Serikali ikitokomeza hii biashara bila ku-provide alternatives kwa wanufaika wake maana yake hasira za hao wanufaika watazimalizia kwenye sanduku la kura. Hii sio kwenye ukahaba tu hata haya makanisa uchwara yaliotapakaa mitaani serikali inaona lakini kwa sababu serikali inahitaji population kubwa ya watu waliokua brainwashed kuukubali unyonge inaamua kuyaacha hayo makanisa yaendelee kuwepo maana dini ni nyenzo nzuri ya kumfanya mtu akubaliane na umasikini, ufisadi unaofanywa na viongozi n.k kwa ahadi ya kwamba ataishi vizuri ukifika mbinguni na hao mafisadi watatupwa motoni wakifa. Mambo mengi serikali inaona lakini kwa sababu kuna namna inanufaika nayo inaamua kukaa kimya tu, serikali ni kikundi cha wanasiasa tu wanaangalia masilahi yao. Wajibika na familia yako