Kanisa Katoliki kwa miaka nenda rudi wamekuwa na utamaduni wa kujilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi nchi mbalimbali, na ardhi hiyo huwa inasauiliwa Vatican kama milki yao halali.
Kanisa limekuwa likifundisha kwamba tusijiwekee akiba duniani, lakini lenyewe ndio kinara wa kujilimbikizia ardhi.
Mathayo 6:19-20
“Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba."
Haya mafundisho naona yanakinzana na kile ambacho kanisa linakifanya. Sasa ningependa kujua nini dhamira ya kanisa kumiliki haya maeneo makubwa? Kijijini ni mfano tu, kanisa linamiliki zaidi ya heka mia mbili, za nini zote hizi kama sio ulafi tu na ubinafsi?
Hebu tujulishane nyuma ya mpango huu kuna nini kilichojificha?
Kwanini ardhi isajiliwe kama ni mali ya Serikali ya Vatican?
1. Unapolituhumu Kanisa Katoliki "kujimilikisha ardhi" inabidi uwe na mifano halisi ili hoja yako isimame yenyewe.
2. "Kujimilikisha ardhi" ni dhana hasi - "land grabbing" - kuchukua ardhi ya mtu au ya umma bila kuwa na haki ya kufanya hivyo.
3. Kanisa Katoliki katika sehemu mbalimbali duniani inamiliki ardhi kihalali - 1) ama kumiliki ardhi kwa sheria ya kimila (mfano, kufyeka pori ambalo halijatumika, ambayo kisheria ni njia mojawapo ya kumiliki ardhi) au 2) kumiliki ardhi kwa kupata hati miliki (title deed).
4. Ardhi yote inayomolikiwa na Kanisa Katoliki si mali ya papa, kardinali, askofu, padri, katekista, kiongozi etc, bali ni mali ya walei na ni kwa ajili ya mahitaji ya huduma za kanisa - kujenga shule/chuo, hospitali, vituo vya kulelea watoto, karakana kwa ajili ya mafunzo stadi ya vijana na pia kwa ajili ya makazi ya wananchi wanaozunguka eneo la Kanisa. Mfano, wakazi wengi wa maeneo ya Kanisa Katoliki wamepewa ardhi na kujenga makazi yao na kama siku moja kanisa litahitaji kuchukua ardhi kama hiyo, litawafidia hao wananchi kwa muda wote ambao wameendeleza ardhi yao.
5. Ardhi inayotolewa kwa Kanisa Katoliki haitolewi na kumilikiwa na Vatican, bali na kanisa parokia au jimbo (kanisa mahalia).
6. Huna ushahidi wowote unaoonyesha kwa mfano hivi karibuni tumemilikishwa ardhi ya kujenga kigango maeneo ninapokaa hapa Dar es Salaam na kwenye hati hakuna jina la Vatican.
7. Yesu aliposema 'msijiwekee hazina hapa duniani' (Mathayo 6:19-20) hakuwa na maana kwamba watu au Kanisa lisimiliki ardhi, bali kwamba umiliki wao wa ardhi usije ukawa chanzo cha kumsahau Mwenyezi Mungu (mfano anayepora ardhi ya watu kwa masilahi binafsi amemsahau Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu anataka utende haki na siyo kuwaibia au kuwanyonya watu).
8. Badala ya kujenga hoja inayoeleweka, hapa umeamua kutulisha 'matango pori' kwa sababu umeshtumu tu na hujaonyesha kwa ushahidi ni kwa jinsi gani Kanisa limewapora watu ardhi au limepora ardhi ya umma kwa kutumia Vatican. Hivyo, yako ni "hoja zoa zoa".