DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Ndyo Ni kweli na Kwa Mujibu wao wako sahihi kabisa..Hilo liko wazi na hakuna asiyefahamu kuwa wayahudi waamini mungu mmoja tu,ila bado wana amini kuwa masihi atakuja kuwakomboa so bado wanasubiri masihi.
Nataka nikuulize wewe Unamuamini joseph Smith Kuwa Ni Nabii na Mtume wa Mwisho kutoka kwa Mungu na alikutana na Yesu Marekani na Yesu akampa kitabu??
Ambacho ndiyo biblia ya wamormons Mpaka Leo??
Umewahi kuisoma Biblia ya Mormons?
Kama hujawahi kwnini?
Unawa Consider wa Mormons kama ni wakweli?
Na Vipi kuhusu Itikadi yao ya Kidini?
Kama huwaamini wamormons kuhusu Imani mpya walioleta kuhusu Yesu na Vingine kwanini Unataka Wayahudi Waamini Kuhusu Yesu na Bado kwa mujibu wao Hajafit Vigezo walivyokuwa navyo Kwenye Utabiri na Unabii wao..
Kama ambavyo wakristo hawamuaminj Mtume Muhammad Kama Mtume wao na hawaamini Uislmu kadhalika ni sawa kwa wayahudi Kutoamini kuhusu Yesu