Ipo haja ya kumuombea Magufuli msamaha, lawama ni nyingi mno

Kama ibilisi mpaka anaingia motoni kashindwa kukiua hicho chama, ndio mtaweza nyie wauza sura hivi sasa?
 
Kwa magufuli tulipigwa ndiyo maana God akatuondolea hilo balaa
 
Kwa kosa gani? Huo msamaha baki nao mwenyewe. Alitimiza majukumu yake ya kikatiba na kuleta maaendeleo kwa spidi kubwa hadi kifo kilipomchukua. Staili yake ya uongozi haikuwa ya blabla na maneno matamu mliyozoeshwa bali vitendo vyenye matokeo tu.
Viwanda alivyokuwa ana danganya vipo wapi
 
Mkuu una hoja ya msingi, sasa unaonaje ukitoka nyuma ya keyboard ukaingia mtaani hata hapo ulipo mtaani kwenu ukawakusanya watu halafu uwaambie ujumbe huu huu uliotuletea hapa, halafu utuletee mrejesho na kavideo pia katapendeza. Maana binafsi nauona huo moyo wako wa kuhamasisha watu wengi wenye hisia kama yako washiriki jambo hili, basi ingia field sasa mzee. Au ukishindwa kuwakusanya watu mtaani basi chagua basi lolote au kwenye mwendokasi uwafikishie watanzania wenzetu ujumbe huu ili nao ambao washiriki hilo suala.
 
Kama ibilisi mpaka anaingia motoni kashindwa kukiua hicho chama, ndio mtaweza nyie wauza sura hivi sasa?
chama kipi unazungumzia hiki,kinachochangisha buku buku kujenga viosk 2021!![emoji16][emoji16].

propaganda zimeshakulemaza wewe.
 
chama kipi unazungumzia hiki,kinachochangisha buku buku kujenga viosk 2021!![emoji16][emoji16].

propaganda zimeshakulemaza wewe.

Hicho hicho cha buku buku, hebu waambie TLP wachangishe hizo buku buku uone kama watapata hata laki 5
 
Hicho hicho cha buku buku, hebu waambie TLP wachangishe hizo buku buku uone kama watapata hata laki 5
kama leo hii kilichokuwa chama kikuu cha upinzani kinatajwa na TLP pamoja,nina kosa lipi nikisema kimeshajifia!!!

2021 twende na mama,2025 kila mtu akale alipopeleka mboga.
 
JPM amekosea nini kikubwa hivyo cha kuombewa msamaha? Hivi kwani yeye tu ndio ana dhambi?Pengine alikuwa mkali na katili kwa wapinzani wake..lakini anayeiba dawa za wagonjwa na kuruhusu wenye dhamana kuiba maoi ya umma naye hatakiwi kuombewa msamaha? Au sababu wanaoibiwa wengi hawana platform kama hizi sababu hawakusoma?
Anayetumia nafasi ya umma au cheo chake kunufaisha kwa hila familia yake na rafiki zake hatakiwi kuombewa msamaha? Kwani ndio kazi aliyotumwa kuifanya?
Sote ni wakosefu wa aina moja au nyingine. Tunakatazwa kuhukumiana maana hata sisi tuna makosa. Kipimo kile kile tunachopimia wenzetu, ndio na sisi tutapimiwa.
Tumuache JPM apumzike kwa amani. Tupambane na changamoto zetu. Hakuna kitu kibaya kama kujidanganya nafsi. Mwenyezi Mungu huwa hadanganywi
 
kama leo hii kilichokuwa chama kikuu cha upinzani kinatajwa na TLP pamoja,nina kosa lipi nikisema kimeshajifia!!!

2021 twende na mama,2025 kila mtu akale alipopeleka mboga.

Kwani tofauti ni ipi, maana sasa hivi ccm inatajwa na chama cha interhamwe.
 
Kwani tofauti ni ipi, maana sasa hivi ccm inatajwa na chama cha interhamwe.
ccm ndio chama dola mkuu,haijalishi unakichukia au unakionea wivu.

moja ya kosa kunwa mnalolifanya ni kuruhusu wanaharakati utumbo twitter na jf kumtukana jpm,mkidhani kuna nafuu mnaleta kwenye chama.

but sio ishu maana mnajua mambo yameshaharibika,bora kumalizia hasira kwa marehemu tu.
 
Too late, alishatangulia mbele ya haki, huko atamalizana na Muumba wake.

Cha kujifunza tuangalie jinsi tunavyoishi duniani na wenzetu hata tukiwa juu sana tusijisahau maana hatujui siku wala saa tutakayorudi kwa Muumba wetu !
Maviongozi huko serikalin ni mapuuz sana..yaani hayabadiliki...

Viburi, yaani magu aliwafaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…