Wasalaam wajumbe wa jukwaa hili!
Naomba kudeclear kabisa kua mimi ni Mwanaccm toka 1997, nachozingumzwa hapa naomba nisipelekwe ufipani.
Ninachoshangaa na wanaccm wenzangu kujawa hopes kua tunaweza kushinda uchaguzi huu kwa urahisi hivyo, naomba ni waambieni kwa ushahidi huu kua Lissu ni kisiki kizito mara 10 ya Dr Slaa wa 2010 au LOWASSA wa 2015.
KWANINI LISSU ANAWEZA KUSHINDA?
Nikikumbuka na ya kuyafikiria haya ninashauri kabisa CCM tusibweteke na kujisahau.
1.Mwaka 2010 Tundu Lissu aliwahi kushinda ubunge katikati ya ngome ya CCM mkoa wa Singida na kujinyakulia Jimbo la Singida mashariki huku akiwa na madiwani 3 tu kati ya 17. Awamu iliyofuata 2015 alishinda tena na kuchukua kata 16 za madiwani akipoteza 1 tu.
2. Kuna wabunge wa CHADEMA wenye kauli kali sana za kujiamini na zisizoogopa mtu kama vile Mbowe, John Mnyika, John Heche,Godbless Lema na Halima Mdee, tujiulize kama kweli watanzania hawapendi kauli kali kwanini wabunge hawa mpaka leo hawajawahi kushindwa kwenye majimbo yao?
Kama watanzania wanapenda kauli za ukali basi Lisu anaweza kutoboa na lazima tufahamu kua ukali wa Lissu na Dr Mafufuli ni tofauti kidogo, Lissu anazidi kidogo ukali na Ukali wake ni unaambatana na sequences zenye facts za kisheria na hivi ni mtaalam wa sheria.
3. Kwanini hatuelewi kuwa Lissu ni mwanasheria mbozi, huu ushindi wa mezani wa kupita bila kupingwa tunajua atawashauri na kuwasomesha nini wagombea wa ubunge na udiwani?
Badala ya sisi kuweka mapingamizi basi tutakuta wao wametujazia mapingamizi.
Mkitaka kulijua hili muulizeni kuja jamaa moja anaitwa Wilson Nkhambaku mwaka 2010 alipohama CCM na kujiunga CHADEMA jimbo la Singida Magharibi baada ya kuonewa kwenye kura za maoni ccm, tulikimbilia kumwekea pingamizi lakini alichokifanya Lissu tunakijua mpaka huyo jamaa kupewa nafasi ya kugombea?
4.Niwaambieni kua Tundu Lissu ni zaidi ya jeuri kwenye mikakati ya uchaguzi, huyu ndiye aliyewashauri CHADEMA wenzake kua muda umeenda waachane na kulia na tume huru ya uchaguzi, aliwaambia "Tutashinda kwa tume hii hii pamoja na mapungufu yake".
Je, kuna nini hapo?
5.Jimbo la Singida Mashariki ni moja ya majimbo mengi Tanzania ambalo madiwani wake wote ni CHADEMA, Pamoja na jimbo kuchukuliwa Lissu akiwa ICU na kupewa Jamaa yetu moja wa CCM aitwaye Miraji Mtaturu lakini hakuna diwani hata mmoja aliyeunga mkono juhudi, tunajua Lissu aliwaambia nini?
Tukubali tuukatae ni lazima tuelewe kua uchaguzi huu wa mwaka huu siyo wa kawaida.
Magufuli ameathiri negatively maisha ya Watanzania wote kwa maamuzi yake ya chuki na kibaguzi.
Miaka 5 iliyopita Upinzani hawakuruhusiwa kufungua mdomo wakati wenyewe CCM waliendelea na kampeni. Kitu ambacho Magufuli alidhani anaua upinzani. Kinyume chake amejenga appetite kwa wa -Tanzania kusubiri wapinzani wateme nyongo.
Sioni Magufuli akipata hata 30% ya kura. Atapata kura za akina Makonda na ndugu zake wa Chatto anaowapa uteuzi kila siku.
Wa Tanzania wote au wenyewe au ndugu zao amewaathiri kimaisha kwa maamuzi haya:-
-Kuwaondoa wanafunzi wa UDOM
- Kufuta wafanyakazi wa vyeti feki
- Kuwatumbua wafanyakazi bila kufuata sheria
- Kutopandisha mshahara na madaraja
- Kutotoa ajira kwa wahitimu wa vyuo
- Kuvunja nyumba za Kimara na kuachia za Mwanza
- Kubagua maendeleo majimbo ya wapinzani kama Kilwa
- Kuzuia wanafunzi wenye mimba wasiendelee na masomo
- Kumtimua CAG makini
-Kuua wakosoaji kama BenSaa Nane na Azory Gwanda
- Kutumia vibaya fedha za Serikali kama ujenzi wa kiwanja cha Ndege Chato
- Kuwaweka rumande wafanyabiashara kwa makosa ya kubambikiza kama Rugemalira
-Kuwabambikiza makosa wakosoaji kama Kabendera
- Kutunga sheria kandamizi
-Kutawala kwa kidikteta
- Kufanya maamuzi bila kushirikisha Baraza la mawaziri
Hayo ni baadhi tu!!