Ndugu Mahanju,
Kwanza nikushukuru sana, nimesoma post yako ambayo ni very interesting, na ina facts nyingi.
Mimi ni a member na a big supporter wa CCM, na niko very very proud, lakini sio mshabiki wa kufunbia macho yasiyo pendeza au haki kudhulumiwa itendwapo na watu wangu na nikafurahia, apana nitakataa na kupinga uovu hata ndani ya nyumba yangu. Na always nitasherehekea lolote zuri linalofanywa na mtanzania au mwanadamu yoyote.
Katika point zako zote ninapinga hii hapo chini:
2. Kuna wabunge wa CHADEMA wenye kauli kali sana za kujiamini na zisizoogopa mtu kama vile Mbowe, John Mnyika, John Heche,Godbless Lema na Halima Mdee, tujiulize kama kweli watanzania hawapendi kauli kali kwanini wabunge hawa mpaka leo hawajawahi kushindwa kwenye majimbo yao?
Kama watanzania wanapenda kauli za ukali basi Lisu anaweza kutoboa na lazima tufahamu kua ukali wa Lissu na Dr Mafufuli ni tofauti kidogo, Lissu anazidi kidogo ukali na Ukali wake ni unaambatana na sequences zenye facts za kisheria na hivi ni mtaalam wa sheria.
Tukubali tuukatae ni lazima tuelewe kua uchaguzi huu wa mwaka huu siyo wa kawaida.
Bw. Mahamju, Kauli kali sio sababu kuu au muhimu ya kumpandisha mtu au kumshusha, Ushindi wa wabunge wengi wa upinzani katika majimbo, unatokana na maono ya wananchi, upevukaji wa kisiasa na Zaidi ulikuwa ni uzembe wa chama cha CCM, kwani walijipa na kutegemea kwa vyovyote watashinda, Na chadema ya wakati huo, tusisahau kuwa mikakati ya ushindi wa hao wabunge uliowataja , ili wekwa na watu makini kama akina Zitto, Kitila na wengineo ambao leo hawapo chadema, na waliogozwa na DR.Slaa, Chadema walikuwa na very visionary team ambayo imesambaratishwa na umimi .
Ndugu Mahanju, wachache wetu tumeishi njee ya nchi na wengine bado tuko huko, tusijaribu, kuleta siasa za nchi za ulaya hapa kwetu , hazitapokelewa vizuri na haziendani na mila zetu, watu wetu hawana uwezo wakimaisha (Financial support) na kuweza kufanya mgomo kwa siku mbili mfulilizo, they cannot be on the street Zaidi ya masaa mawili, na Zaidi ni kwa sababu hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kujitolea, kama alivyokuwa Dr.Slaa, tusijidanganye, kila mmoja anachunga kivuli chake.
LISSU ni mzungumzaji mzuri, but haimfanyi mwanasiasa mzuri, siasa za fujo hazina mueleko wala hazitapokelewa,Upinzani wanijua solution, lakini hawana ubavu walifikia hilo kwa sababu ya UMIMI/ SELFISHNESS na uroho wa mali na madaraka.
Ni kweli yako Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na kelele na kashfa nyingi, Lakini tusije shangaa matokeo yasipokuja kuwa kama upinzani wanavyofikiria.